Kanye West amefunua tukio la unyanyasaji wa kingono ambalo mkewe, Bianca Censori, anadaiwa kulipitia katika hoteli ya Chateau Marmont huko Los Angeles, California.
Kwenye mahojiano na Justin Laboy kwenye podcast ya The Download, Kanye West alielezea hatua za haraka alizochukua baada ya kupokea taarifa za tukio hilo alilofanyiwa mkewe.
West alipata habari kwamba mtu fulani alikuwa amemkabili mkewe wakati alipokuwa akielekea bafuni. Kwa mujibu wa West, alikwenda haraka kumsaidia mkewe na kumkabili mtu huyo, akimtaka kuondoka mara moja katika eneo la karibu na Hoteli hiyo alipo mkewe.
Hata hivyo, mtu huyo alikataa kuondoka, na West aliamua kumshambulia, akimlazimisha kulala chini. Ushuhuda wa mashuhuda wengine wa tukio hilo unapingana na madai ya West.
Mashuhuda hao walisema kulikuwa na mgongano wa bahati mbaya kati ya mwanamke na mtu huyo, ambayo ilisababisha West kumkabili nje ya jengo hilo.
Ingawa inaonekana West alimpiga mtu aliyehusika na tukio hilo, inasemekana alimpiga ndugu yake badala yake. Wawakilishi wa West wamesisitiza kwamba Censori alishambuliwa kimwili na kufanyiwa unyanyasaji wa kingono.
Walielezea jinsi mshambuliaji alivyomkamata chini ya vazi lake na kumpelekea busu, huku wakieleza kuwa Censori alipigwa na kufanyiwa unyanyasaji wa kingono.
Hadi sasa, Censori hajawasilisha mashtaka ya jinai dhidi ya watu hao wawili. Habari hii inaendelea kufuatiliwa kwa karibu, na kuna matarajio ya kupata maendeleo zaidi kutoka pande zote husika.
Wakati huo huo, umma unaendelea kusubiri kwa hamu kujua ukweli uliopo nyuma ya tukio hili la kushtua na lililokonga hisia za wapenda burudani na mashabiki wa nyota huyo wa marekani asiyeishwa na Matukio kila kukicha kwenye Maisha yake.
Habari hii itaendelea kufanyiwa uchunguzi na hali ya Censori inaendelea kufuatiliwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa.
Your article helped me a lot, is there any more related content? Thanks!
I don’t think the title of your article matches the content lol. Just kidding, mainly because I had some doubts after reading the article.