Jeshi la Polisi Nchini, limesema linatalajia kuwa, mwenyeji wa zoezi la mafunzo ya utayari kwa vitendo (Field Training Exercise – FTX) mwaka 2024 litakalojumuisha nchi 14 wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Ukanda wa Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) kuanzia tarehe 13 – 18, Aprili 2024.
Akitoa tarifa hiyo leo Aprili 11,2024 Msemaji wa Jesh la Polisi Nchini naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema Zoezi hilo la pamoja linatarajiwa kufanyika katika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi ambapo takribani Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wapatao 670 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo.
Read>> Polisi Kuimarisha Ulinzi Kuelekea Sherehe Z a Pasaka
https://mediawireexpress.co.tz/polisi-kuimarisha-ulinzi-kuelekea-sherehe-z-a-pasaka/
DCP Misime amebainisha kuwa Kufanyika kwa mazoezi hayo kunatokana na maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Shirikisho la Polisi Ukanda wa Mashariki mwa Afrika katika mikutano yao ya kila mwaka.
Ameongeza kuwa Katika mkutano uliofanyika mwezi Oktoba, 2021 Kinshasa nchini Kongo, Wakuu hao wa Polisi walipitisha azimio la zoezi hili kufanyika hapa nchini.
Pia amezitaja Nchi zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na mwenyeji Tanzania, Burundi, Eritrea, Djibouti, DRC Kongo, Kenya, Komoro, Ethiopia, Shelisheli, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudani Kusini na Uganda.
Read>> Polisi na TBS kufunga Mitambo ya kisasa Mipakani
https://mediawireexpress.co.tz/?s=polisi
Msemaji wa Jeshi hilo amebainisha kuwa zoezi hilo litafanyika katika shule ya kipolisi Tanzania iliopo Moshi ,Lengo la mazoezi mengine yaliyopita ni kuwajengea Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali uwezo wa kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu unaovuka mipaka kama vile ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, Biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na kubadilishana uzoefu na taarifa za kitelejensia.
DCP Msime amesema maandalizi ya zoezi hilo yameanza kukamilika kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa (Interpol) kanda ya Afrika mashariki na kuwataka wananchi kudumisha utamaduni wao wa kukarimu wageni wanapokuja nchini.
I am continually browsing online for articles that can benefit me. Thank you!