Dark
Light

Polisi Kuimarisha Ulinzi Kuelekea Sherehe Z a Pasaka

machi 31,2024 Waumini wa Dini za Kikristo wataungana na wenzao Duniani katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka huku likibainisha kuwa limeimarisha ulinzi na usalama kuelekea sikukuu hizo.
March 27, 2024
by

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema machi 31,2024 Waumini wa Dini za Kikristo wataungana na wenzao Duniani katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka huku likibainisha kuwa limeimarisha ulinzi na usalama kuelekea sikukuu hizo.

Akisema hayo DCP David Misime wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari mkoani Arusha leo 27, Machi 2024 akibainisha kuwa  Sherehe hiyo hutanguliwa na waumini wa dini hizo hukusanyika kwa wingi na kushiriki Ibada ambazo hufanyika nyakati za mchana na usiku,siku za Alhamis,Ijumaa,Jumamosi na Jumapili na Jumatatu ya Pasaka.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kujiimarisha ulinzi na kuhakikisha kwamba ibada na sherehe hizo zinafanyika katika hali ya amani, utulivu na usalama wa kutosha ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limejipanga kufanya doria katika mitaa na barabara zote kuu ili kuzuia uhalifu au uvunjifu wowote ule wa amani.

Sambamba na hilo amesema katika barabara zote kuu, kutakuwa na doria za Askari ili kuzuia ajali za barabarani, Pamoja na kukagua watakao kiuka sheria za usalama barabarani kama vile kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wakiwa wamelewa pombe na kujaza abiria kupita kupita kiasi.

Msemaji wa Jeshi hilo amesema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Viongozi wa nyumba za ibada ambao watakuwa na ibada katika kipindi hiki cha Juma Kuu wasisite kuwasiliana na Viongozi wa Polisi katika maeneo yao ili washirikiane katika kuimarisha usalama kwa kipindi chote.

Vile vile Jeshi hilo Pia linaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuzingatia kanuni ya kiusalama inayosema “usalama unaanza na mimi mwenyewe”

Pia Pamoja na hilo Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi kuchukua tahadhari na kujiepusha na marafiki wa mitandaoni na matapeli wanaojitangaza kuwa wanatoa mikopo kupitia mitandao.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Dr. Ndumbaro: Globalization Should Not Be Used To Destroy Our Culture

The Minister of Culture, Arts, and Sports, Dr. Damas Ndumbaro,

Tanzania Sees Record Investment Growth Under President Samia

Tanzania has witnessed a remarkable surge in investment over the