Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepanga mwaka 2024/25 kutumia shilingi bilioni 841.19 kwa ajili ya ujenzi, matengenezo, ukarabati wa miundombinu ya barabara na usafiri na usafirishaji wa vijijini na mijini ikiwamo ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa mita 141,070.54 na ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi ili kudhibiti maeneo ya juu ya Mto Msimbazi.
Pia kuhamisha karakana ya mabasi yaendayo haraka kutoka Jangwani kwenda eneo la Ubungo Maziwa.
Read more: Ukarabati Mto Msimbanzi Serikali Yatekeleza Awamu Ya Kwanza
https://mediawireexpress.co.tz/ukarabati-mto-msimbanzi-serikali-yatekeleza-awamu-ya-kwanza/
Haya yamebainishwa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa Wizara hiyo, Sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa na taasisi zake.
Amesema kati yaa fedha hizo Sh. bilioni 257.03 ni za Mfuko wa Barabara, shilingi bilioni 127.50 Mfuko Mkuu wa Serikali, Sh. bilioni 325.77 ni za tozo ya mafuta ya petroli na dizeli ya shilingi 100 kwa lita, Sh. bilioni 4.03 za mapato ya ndani kupitia Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam na Sh bilioni 126.85 ni fedha za nje.
Mchengerwa amebainisha shughuli ambazo zitakazotekelezwa kuwa ni utunzaji wa barabara za vijijini na mijini zenye urefu wa Km. 20,745.31, ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 434.50, ujenzi wa barabara za changarawe zenye urefu wa kilomita 13,802.34, ujenzi wa madaraja 160 na ukarabati wa madaraja 21 na ujenzi na matengenezo ya boksi kalavati 586 na vivuko 15.
Read more: Tamisemi yaomba Sh10 trilioni ikitaja vipaumbele saba
Pia kuboresha Miundombinu Shindanishi katika Miji Tanzania (TACTIC) kwa kujenga miundombinu katika Halmashauri 12 za Majiji ya Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya na miundombinu msingi inajumuisha ujenzi wa masoko, mitaro ya maji ya mvua, stendi za mabasi, maghala ya kuhifadhia mazao na kujenga barabara kiwango cha lami kilomita 147.5.
Pia kuondoa vikwazo vya upitikaji barabarani kwenye wilaya 131 na ujenzi wa barabara kiwango cha lami Awamu ya Pili kilomita 164 kupitia Programu ya Kuongeza Fursa za Kiuchumi na Kijamii Nchini (RISE), ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 250, kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya 2 ambapo kati ya hizo kilomita 132 zimefanyiwa usanifu na kukamilisha utaratibu wa ununuzi