Serikali imekili kuwa gharama za dawa za kutibu maji ni kubwa na imewaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa hiyo itakayo punguza gharama za upatikanaji maji nchini.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema akiwa London, Uingereza kushiriki Mkutano wa 13 wa ubunifu wa teknolojia za maji mwaka 2024(World water Tech innovation summit) iliyoanza Februari 19 hadi 21 Februari 2024.
“Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Re Think Events kwa kushirikiana na Idara ya Biashara za Kimataifa ya Serikali ya Uingereza umewaunganisha wadau wa Sekta ya Maji duniani wakiwemo Wafadhili na Makampuni yanayozalisha vifaa vya maji, teknolojia za maji pamoja na madawa ya kutibu maji” amesema Mahundi
Amesema kupatikana kwa wadau kutoka Taasisi na Makampuni ya kimataifa yatakayowekeza katika viwanda vya kuzalisha madawa ya kutibu maji nchini kutaimarisha huduma za maji kupitia kupunguza gharama za madawa na kuimarisha uchumi wa Taifa kupitia ajira kwa Watanzania miongoni”amesema
Hata hivyo Programu ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji Tanzania ni ya miaka nane 2023 – 2030 ambayo itahusisha miradi ya uwekezaji inayohusiana na maji yenye thamani ya takriban Dola za Marekani Bilioni 20.6 na itaongeza wigo wa wadau wa maendeleo na kuongeza bajeti ya ndani kwa ajili ya kuimarisha uwekezaji katika Sekta ya Maji.
Wow! Thank you! I continually needed to write on my blog something like that. Can I implement a fragment of your post to my website?
Muchas gracias. ?Como puedo iniciar sesion?