Mashabiki Wa Simba Wametoa Neno Juu Ya Matokeo Ya Timu Yao Baada Ya Kufurumushwa Kwenye Michuano Ya Ligi Ya Mabingwa Afrika Pamoja na CRDB Confederation Cup.
Mashabiki Hao Waliopo Kawe Kanisani,Wamezungumza Na Media Wire Na Kueleza Ni Jinsi gani Mwenendo wa Matokeo Mabovu Unawaaumiza Sana Kwani Matarajio Yao Yalikuwa Makubwa kwa Wachezaji Pamoja Na Uongozi Wa Klabu Juu ya Malengo ya Kuchukua Ubingwa Wa Ligi Kuu na Kombe La shirikisho (CRDB FA Cup) Pamoja Na Kufika Nusu Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Afrika Lengo Lililogonga Mwamba Takribani Misimu Mitano iliyopita.
Read: “Simba Imeingia Mtegoni,Watu Waongeza Chumvi”-Ahmed Ally
https://mediawireexpress.co.tz/simba-imeingia-mtegoniwatu-waongeza-chumvi-ahmed-ally/
“Simba Inamatatizo Mawili Ambayo Ni ndani ya Uwanja Pamoja na Nje ya Uwanja, Tukianza Ndani ya Uwanja ,Simba Haina Mshambuliaji Wakutegemewa Kutuhakikishia Magoli Mengi Zaidi ya Tulivyo Sasa Hivi, Pili Ni Uongozi Wa klabu ,Kuanzia Mo ,Mangungu,Try Again na Wajumbe wao,
Mfano Walimleta Manzoki Hapa kipindi Cha Uchaguzi, Lakini Aliletwa Kama Nyoka Wamaonesho Kutuzuga, Milioni Mia Nne iliwashinda Nini Kutoa Wakati Mo Kwa Mwaka Anatoa Takribani Bilioni Tatu Kwenye Bajeti Ya Simba?” Saidi Ally, Shabiki Wa Simba.
Pia Mashabiki Hao Wamesema Hata Kama Timu Yao Haipo Katika Wakati Mzuri Uwanjani, Lakini Linapokuja Swala La Derby Ya Kariakoo Si Rahisi Tena Kufungwa Na Yanga.
“Game (Mechi) Itakuwa Ngumu,Ingawa Simba Ni Mbovu Lakini Haitokuwa. Mechi Rahisi Na Yanga, Zile Goli Tano Wasizitegemee Kabisa ,Timu Itapambana Kushinda”Amina Ally, Shabiki Wa Yanga
Read: Simba Yatozwa Faini Milioni 1 Shabiki Kufanya Vitendo Vya Kishirikina
https://mediawireexpress.co.tz/
Nao Watani wao Wa Jadi Yanga Wamewaomba Mashabiki Wenzao Na Hata Timu na Uongozi Wao Kuelekeza Nguvu zote Kwenye Kuchukua Ubingwa Wa Ligi Juu ya NBC Pamoja na Kombe la Shirikisho Yaani CRDB FA Cup, ili Kufikisha Kilele Cha Malengo Ya Timu Yao Msimu Huu.
” Sisi Tuachane na Hawa Mmakolo(Klabu Ya Simba) Tupambane na Ligi Kuu Na Shirikisho Tufikie Malengo Ya Msimu, Wao Waache Wanengenege Hivyo Hivyo”Said Athumani,Shabiki Wa Yanga.
Excellent website. A lot of helpful information here. I am sending it to several buddies ans also sharing in delicious. And naturally, thank you on your sweat!
I got what you mean ,saved to fav, very nice internet site.
I view something really special in this web site.
Thank you for your sharing. I am worried that I lack creative ideas. It is your article that makes me full of hope. Thank you. But, I have a question, can you help me?
Thanks for sharing. I read many of your blog posts, cool, your blog is very good.