Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga Mrisho Ngassa ameposti katika ukurasa wake wa instagram kujibu tuhuma za mchezaji mwenye asili ya Congo Fiston Mayele ,kufuatia tuhuma zilizotolewa jana Feb 12,2024 asubuhi.
Katika ujumbe wake huo Ngassa amesema “Kuna kipindi niliamia team nyingine kutoka Yanga nikakuta kule mashabiki wachache, nishazoea shangwe kufunga kukawa shida nikasema ndio nimeisha au lakini sikuwaza majini, Kuna wachezaji wakitoka Simba, Yanga au Azam kufunga ni ngumu wanaenda team Mashabiki wapo 30 mpinzani aogopi chochote uwezo wako ndio watakiwa uwonyeshe.”
“Sasa umeondoka katika team umeuzwa watu wamepiga pesa wamefurahi unakuja umetupiwa jini Basi Fei Ttoto Angekuwa chizi, majini ya kusafiri na majini ya hapa hapa yanamuona, team ni kubwa kuliko mtu yoyote hii ni story fupi wachezaji Kuna maisha baada ya soccer tuishi vizuri na shule tulizo pita kesho tutasomesha watoto wetu Kwa Ada ndogo” Ngassa.
Hayo yamejiri baada ya jana kuibuka sintofahamu kufuatia ujumbe wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Fiston kwenye mtandao wa Instagram ulisomeka “Chuki ya nini mimi sio Mtanzania,nilikosea kucheza timu ya Tanzania ” akionesha kuumizwa na kitu na kuwataja mashabiki wa Yanga alipojibu moja ya ‘comment’ ya shabiki yake.
Mayele ambaye kwa sasa anachezea Pyramids ya Misri ameonesha kuwa na mengi ya kuzungumza na kuwataja mashabiki wa Yanga kuwa anawajua vizuri tabia zao