Korea Kusini imezuia video kadhaa zinazoonesha wimbo mpya wa propaganda wa Korea Kaskazini unaomsifu Rais wa nchi hiyo Kim Jong Un ambao umethibitishwa kuwa maarufu bila kutarajiwa nje ya nchi hiyo, hatua ambayo wataalam wanaiita uharibifu wa uhuru wa kidemokrasia.
Tume ya Viwango vya Mawasiliano ya Korea (KCSC) ilitangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumatatu kwamba Kamati Ndogo ya Mapitio ya Mawasiliano iliomba kuzuia video 29 za wimbo “Mzazi Rafiki” au”Baba Rafiki”
Video hiyo iliyooneshwa kwa mara ya kwanza kwenye runinga ya serikali katikati ya mwezi wa Aprili, ilionesha matukio ya uongozi wa Kim Jong Un na picha za wanajeshi waliojawa na furaha na raia wakionesha kumuunga mkono kwa ishara za dole gumba.
Soma Zaidi:Putin gifts luxury Aurus car to North Korea’s Kim
Mdhibiti wa vyombo vya habari wa Seoul alisema video hiyo ya muziki, ambayo imekuwa maarufu kwenye TikTok tangu ilipotolewa Aprili, ni ukiukaji wa Sheria ya Usalama wa Kitaifa ya nchi hiyo.
“Video inayozungumziwa iligunduliwa kukiuka Sheria ya Usalama wa Kitaifa kwa kuabudu na kumsifu Kim Jong Un kwa maneno yanayomwita ‘mzazi rafiki’ na kumwelezea kama ‘anayewakumbatia na kuwajali wakazi wa Korea Kaskazini kwa upendo” taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilieleza.
Ikiwa imepitishwa mwaka wa 1948, Sheria ya Usalama wa Kitaifa (NSA) ilipiga marufuku kushiriki maudhui ya Korea Kaskazini na kuzuia ufikiaji wa tovuti za DPRK nchini Korea Kusini, huku baadhi yao wakikosoa sheria kwa kuzuia uhuru wa Wakorea Kusini.