Msanii mashuhuri wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo, ameongoza hoja kali dhidi ya utaratibu unaotumika katika utoaji wa tuzo katika tasnia yao. Katika maoni yake yaliyoenda viral, Marioo ameeleza kuwa hali ya kutokupokea tuzo yoyote katika msimu uliopita inachekesha na kuudhi kwa wakati mmoja.
Marioo amebainisha kuwa anasikia kuna fitna na upendeleo unaojitokeza katika mchakato wa utoaji wa tuzo hizo. Amesema hana hata furaha ya kupokea tuzo ambazo anajua mwenyewe hakustahili kupata. “Nawauliza waandaaji wa hizi tuzo, kwa nini mnatoa tuzo kama hazitendi haki? Mnaombaje ushauri kuhusu tuzo kwa wanaoshindania tuzo hizo hizo?” alisema kwa hasira.
Pamoja na kulaumu utaratibu huo, Marioo amebainisha kuwa hali hiyo inasikitisha na kukatisha tamaa kwa wanamuziki wengine. Amesema kuwa wao kama wanamuziki wanafanya kazi kwa bidii ili kuipa sura nzuri tasnia yao, lakini mchakato duni wa utoaji wa tuzo unawafanya wapoteze ari na motisha.
Soma:Mafanikio ya Burna Boy Yamzuia Kuwa na Watoto Kwa Sasa
Marioo ameutaka utaratibu huo wa utoaji wa tuzo kupitiwa upya ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka na wanaopata tuzo ni wale wanaostahili. Amesema kuwa waandaaji wa tuzo hizo wanapaswa kujitathmini na kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao.
“That was not fair at all. Inasikitisha na inakatisha tamaa. This time around jipangeni,” alimalizia Marioo katika wito wake kwa waandaaji wa tuzo.