Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya Amesema Serikali kupitia waraka wa Rais wa mwaka 1998 imesema magari yote ya Serikali yanatakiwa kuwa yameegeshwa sehemu zilizotengwa kwa ajili hiyo ifikapo saa 12:00 jioni bila kukosa, vinginevyo kiwepo kibali maalum.
Kasekenya amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo Arumeru Magharibi, Noah Saputu aliyeuliza ni lini Serikali itazuia kupaki magari ya Serikali sehemu za starehe baada ya saa za kazi.
“Serikali kupitia walaka wa Rais namba 1 wa mwaka 1998 kuhusu hatua za kubana matumizi ya serikali ilielekeza kuwa kuegesha magari sehemu zilizotengwa kwaajili hiyo ifikapo saa 12 jioni bila kukosa vinginevyo kiwepo kiwepo kibali cha serikali kuonesha gari inatakiwa iwepo barabarani”
Read>> http://Kamati ya Bunge Yachukizwa Kurejeshwa kwa Mikopo ya KKK
Pia Kasekenya amejibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga,lililosema kuwa “Upi mkakati wa makusudi wa serikali unazuia kabisa uwepo wa magari hayo mtaani maana imekuwa kero kwa wananchi na inaonesha uwepo wa matumizi mabaya ya fedha na uvunjifu wa sheria”
“Tunawakumbusha na kuwasisitiza maafisa masuhuri na waajiri wote sheria zimeelekeza mtumishi yeyote anayemiliki chombo cha umma na hasa magari asiwe barabarani baada ya saa 12 jioni na asiweze kuwa katika maeneo ambayo si sahihi (maeneo ya starehe) kwa muda ambao hauruhusiwi,” Kasekenya
Read>> https://mediawireexpress.co.tz/silaa-aonya-magari-ya-serikali-kubeba-mkaa-maharusi/
Hata hivyo Kasekenya amesema sheria zinazuia watumishi wa umma kutumia magari ya Serikali kwa matumizi binafsi na kuagiza kwa wale watakaokwenda kinyume watachukuliwa hatua za kinidhamu.