Hali ya madeni ni mbaya kwa Real Madrid na hii imepelekea kuanza kuandaa harusi katika uwanja wao wa Bernabeu kama njia mojawapo ya kukusanya fedha ya kulipa mikopo ya mabilioni ya fedha waliyokopa kwa ajili ya kufadhili ukarabati wa uwanja huo.
Kwa mujibu wa Mundo Deportivo Klabu ya Real Madrid sasa ina deni kubwa zaidi kuliko klabu yoyote nyingine barani Ulaya.
Soma Zaidi:Mbappe Aghadhabishwa na Swali
Licha ya kutinga Fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu huu bado timu hiyo imezidi kukimbizana na njia za kupunguza madeni yadaiwayo ikiwa ni pamoja na ujengajiwa uwanja huo pamoja na usajili wa wachezaji wenye thamani katika kikosi
Uwanja wa Bernabeu sasa una ubora wa hali ya juu, ukiwa na miundombinu ya kisasa kama vile paa linalofunguka na kufungwa, mfumo bora wa sauti na mwanga, pamoja na viti vya kisasa kwa ajili ya mashabiki.