Tarehe 1 Mei 2024, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliyotoa taarifa kuhusu uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya Mtwara.
Tangu wakati huo, mgandamizo huo umekuwa ukiongezeka nguvu na kujitokeza kama kimbunga kinachojulikana kama “HIDAYA.” Kimbunga hicho kina nguvu ya kati na kimefikia umbali wa takriban kilomita 506 mashariki mwa pwani ya Mtwara.
Mifumo ya hali ya hewa baharini inaonyesha uwezekano mkubwa wa kimbunga “HIDAYA” kusogea karibu kabisa na pwani ya Tanzania kuanzia usiku wa tarehe 2 Mei 2024 na kuendelea kuwepo hadi tarehe 6 Mei 2024.
Hata hivyo, inatarajiwa kuwa kimbunga hicho kitapungua nguvu baada ya tarehe 6 Mei 2024.
Soma:TMA Yatangaza Kupatwa kwa Jua Leo Jioni
Uwepo wa kimbunga “HIDAYA” karibu na pwani ya Tanzania unaathiri mifumo ya hali ya hewa katika maeneo mbalimbali. Kuna uwezekano wa kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani (ikiwa ni pamoja na visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, na visiwa vya Unguja na Pemba, pamoja na maeneo ya jirani.
Athari hizi zinatarajiwa kuwa kubwa hasa tarehe 3 Mei 2024 kwa maeneo ya pwani ya kusini (Lindi na Mtwara), na kusambaa katika maeneo mengine ya ukanda wa pwani kuanzia tarehe 4 hadi 6 Mei 2024.
TMA inatoa ushauri kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa na wale wanaojihusisha na shughuli za baharini kuchukua tahadhari kubwa. Wanashauriwa pia kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri na tahadhari kutoka TMA. Ni muhimu pia kupata ushauri na miongozo kutoka kwa wataalam katika sekta husika ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na kimbunga “HIDAYA.” TMA itaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa na itatoa taarifa mara kwa mara kila inapobidi.
Hii ni taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwepo wa kimbunga “HIDAYA” karibu na pwani ya Mtwara katika Bahari ya Hindi Mashariki.
Heey tһere! Ι coulɗ have sworn I’ve beеn tо thiѕ site Ьefore bᥙt after browsing tһrough some of the post I
realizedd іt’s new tօ me. Nοnetheless, I’m definiteⅼy glad I found it and I’ll be book-marking and checking back oftеn!
Here is my paցе: afeccion arasamila precio
Loving the info on this site, you have done outstanding job on the content.