Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Cde.Seif Abdul Namtusi amezungumza na waandishi wa habari na kuzungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo yaliyotekelezwa na serikali Wilayani Masasi chini ya ilani ya CCM ya mwaka,2020/ 2025
Aidha, Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Masasi ametumia fursa hiyo kuwaomba Vijana Wilayani humo kuwa na uthubutu kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika mwaka huu mwezi Oktoba pamoja na uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani mwaka, 2025
Katika mkutano na wandishi wa habari mwenyekiti Seif Namtusi kupitia Umoja wa Vijana Wilaya ya Masasi amesema kuwa Vijana wa wilaya ya Masasi hususani wa Chama Cha Mapinduzi unampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo.
Namtusi amesema katika kipindi Cha miaka mitatu Cha Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya maendeleo makubwa katika Wilaya ya Masasi na kuifanya Masasi kuweza kupaa kimaendeleo.
Soma:Kinana Awavaa Chadema,Muungano Watajwa
Namtusi amesema miongoni mwa mambo ambayo yamefanywa na serikali Wilayani Masasi na yanapaswa kupongezwa ni ujenzi wa vituo qa àqqavya afya, Zahanati, hospitali za Wilaya, miundombinu ya barabara, vyumba vya madarasa na Ugawaji wa pembejeo Kwa wakulima ,mbolea za Ruzuku
Upatikanaji wa vifaa Tiba,Dawa na Huduma nzuri kwenye Zahanati,vituo vya Afya na hospitali
Aliongeza kuwa mambo mengine ambayo yamefanywa na serikali Wilayani Masasi ni usambazaji wa huduma ya maji safi na salama hususani maeneo ya vijijini mtandao maji safi umeongezeka Kwa asilimia kubwa
Usambazaji wa huduma ya umeme kufikia asilimia 100 ya vijiji vyote wilayani humo kupitiwa na Mtandao wa umeme
Pia Umoja wa Vijana Wilaya ya Masasi umewapongeza wabunge wote wa majimbo matatu ya Masasi
Masasi mjini, Lulindi na Jimbo la Ndanda kwa jitihada zao za kuhakikisha Wilaya ya Masasi inapiga hatua ya maendeleo na kwamba Umoja huo utaendelea kushirikiana pamoja na wabunge hao Ili kuwaletea Maendeleo wananchi wa wilaya ya Masasi.
I as well believe thus, perfectly pent post! .