Dark
Light

Mtu Anayekiuka Utaratibu Lazima Ashughulikiwe- Bulaya

Kaimu Mwenyekiti wa LAAC Ester Bulaya amesema kamati itahakikisha inasimamia ipasavyo matumizi ya fedha za umma zilizopelekwa kutekeleza miradi kwenye maeneo mbalimbali na hawatakubali Serikali ipate hasara,amezunguza hayo  baaada kikao cha majumuisho ya ziara walioifanya  katika Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro ya ukaguzi wa jengo la halmashauri, ujenzi wa shule ya sekondari na stendi ya Manispaa Machi 21, 2024.
March 22, 2024
by

Kaimu Mwenyekiti wa LAAC Ester Bulaya amesema kamati itahakikisha inasimamia ipasavyo matumizi ya fedha za umma zilizopelekwa kutekeleza miradi kwenye maeneo mbalimbali na hawatakubali Serikali ipate hasara,amezunguza hayo  baaada kikao cha majumuisho ya ziara walioifanya  katika Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro ya ukaguzi wa jengo la halmashauri, ujenzi wa shule ya sekondari na stendi ya Manispaa Machi 21, 2024.

Ameeleza pamoja na kuonekana kwa ubora wa ujenzi wa miradi katika Mkoa wa Kilimanjaro, Kamati ya LAAC inajukumu la kufuatilia fedha za Serikali ili zifuate utaratibu katika matumizi yaliyopangwa kwa kuzingatia miongozi, taratibu na sheria za Serikali na kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI.

“Naibu Katibu Mkuu ( Elimu) mtu ambaye amekiuka taratibu lazima ashughulikiwe nchi hii ni kubwa unapopata fursa ya kusimamia fedha za miradi lazima tusimamie ilete tija kwa wananchi,” amesisitiza Mhe. Bulaya

Aidha Mjumbe wa LAAC, Mhe. Hawa Mchafu(Mb), amesema Kamati imemtaka Mkurugenzi kuhakikisha kasi ya mradi wa jengo la utawala la Halmashauri hiyo inaongezeka na kukamilika ndani ya muda wa mkataba tarehe 28 Machi 2024.

Amesema Kamati imemtaka Mkurugenzi kuhakikisha utekelezaji wa miradi unazingatia sheria, kanuni na taratibu inayotolewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kujenga kulingana na michoro illyotolewa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI.

Pamoja na maekelezo mengine Kamati pia imeitaka Ofisi ya Rais -TAMISEMI ichukue hatua kwa watu wote waliohusika kwa ukiukwaji wa sheria wakati wa kuingia mkataba wa ujenzi wa stendi.

Naye, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Charles Msonde ameahidi Ofisi ya Rais – TAMISEMI itasimamia kwa karibu maelekezo yote ya Kamati iliyoyatoa na yatatekelezwa ikiwamo kuundwa kwa timu ya kufanya tathmini ya ujenzi wa mradi wa stendi ya Manispaa ya Moshi ili hatua zichukuliwe na wananchi wapate huduma.

4 Comments

  1. I and my guys appeared to be following the best tips on the blog and then before long developed an awful feeling I never thanked you for those techniques. These men were definitely totally very interested to read through all of them and have in effect surely been using those things. Appreciate your simply being so thoughtful and then for pick out variety of beneficial issues millions of individuals are really desperate to be aware of. My personal honest regret for not expressing appreciation to sooner.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Four U.S. Soldiers Killed in Lithuania Training Accident

NATO has confirmed that four U.S. soldiers who went missing

Ruto Urges Regional Cooperation to End DRC Crisis

Kenya’s President, Dr. William Ruto, called for a united and