Tanzania imeweka historia ya kipekee katika sekta ya utalii kwa kushika nafasi ya 5 kimataifa kwa kuwavutia watalii zaidi, kulingana na takwimu za Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) kwa kipindi cha miezi ya Januari hadi Machi 2024.
Taifa hili pia limepata sifa kwa kushika nafasi ya kwanza barani Afrika katika suala la kuwavutia watalii kimataifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb), alitoa tangazo hili muhimu leo wakati akichangia mjadala wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, pamoja na Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Juni 26, 2024 Bungeni Dodoma.
Kulingana na Waziri Kairuki, mafanikio haya ya Tanzania katika sekta ya utalii yamechangiwa sana na juhudi za serikali katika kukuza na kutangaza vivutio vya utalii vya nchi. “Kwa takwimu za Benki ya Dunia za mwezi Mei 2024, Tanzania imefanikiwa kupata mapato ya Dola Bilioni 5.75 kutokana na utalii,” alieleza Waziri Kairuki.
Aidha, aliongezea kwamba Tanzania imepata mafanikio makubwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa zaidi ya 96% tangu mwanzo wa utawala wake.
SomaZaidi;Mapambano Dhidi ya Wanyamapori Waka
“Hadi mwezi Desemba 2023, tulishuhudia watalii takribani milioni 1.8 kutoka nje ya nchi, na ongezeko la watalii wa ndani lilifikia asilimia 152%, kufikia milioni 1.9,” alifafanua Waziri Kairuki.
Mafanikio haya yameifanya Tanzania kutambulika kimataifa kama moja ya marudio bora kwa watalii duniani, na kuweka msingi imara wa ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya utalii. Waziri Kairuki aliendelea kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia zaidi watalii na kuongeza mapato ya kitaifa.
Serikali imepokea pongezi kwa mafanikio haya, na Waziri Kairuki alihitimisha kwa kusema kuwa bajeti ya mwaka 2024/2025 inaonesha dhamira thabiti ya serikali ya kukuza uchumi, kuimarisha miundombinu, na kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi.
There are definitely a variety of particulars like that to take into consideration. That could be a great level to carry up. I offer the thoughts above as normal inspiration but clearly there are questions just like the one you convey up where a very powerful thing might be working in trustworthy good faith. I don?t know if finest practices have emerged around issues like that, however I am positive that your job is clearly recognized as a fair game. Each girls and boys feel the impact of only a second’s pleasure, for the rest of their lives.