Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia Mohamed Omary Salahange (37) mkazi wa Rudewa Gongoni wilayani Kilosa kwa tuhuma za kumuua kisha kumzika kwenye chumba walichokuwa wakiishi, mke wake Beatrice Talius Ngongolwa.
Kamanda wa polisi mkoani humo, SACP Alex Mkama amesema jeshi hilo lilipokea taarifa za siri kuhusu mauaji hayo mnamo Machi 21 zilizoeleza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo alitenda kosa hilo na kuhama kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na mkewe.
Jeshi la polisi limeongeza kuwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa mtuhumiwa alikiri kufanya mauaji hayo na aliwapeleka maafisa wa polisi kwenye eneo la tukio ambako jeshi la polisi kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali pamoja na kamati ya usalama wilaya ya Kilosa waliufukua mwili wa mwanamke kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Jeshi hilo linaendelea na hatua zaidi za uchunguzi wa kimaabara ili kukamilisha upelelezi kwa ajili ya hatua za kisheria.
Source: azammedia
Thanks for sharing. I read many of your blog posts, cool, your blog is very good.