Ili kufikia malengo na kuwa na maendeleo kwa vijana ni vema wakajenga tabia ya kuchagua kitu kimoja cha kusimama nacho ambacho watakifanyia kazi na kuwa hodari badala ya kuwa na vitu vingi ambavyo haviwezi kuwavusha kwenye mapambano ya kiuchumi.
Kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira mtaani na ambao wanaweza kujiajiri popote na kutangazika kirahisi kwa kile wanachokifanya.
Soma Zaidi:Mbowe: Tathmini Ya Maandamano Kwa Mikoa 13
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John amebainisha hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya awali kwa Vijana wa kujitokeza Oparesheni miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kikosi 832 Ruvu Kibaha Mkoani Pwani.
Akiwa katika hafla hiyo Nickson alisema kijana anatakiwa kuwa hodari katika fani yake na kuzingatia uaminifu na uhodari Ili aweze kutambulika na kufanya vizuri katika shughuli zake za kujikwamua na maisha badala ya kuwa na vitu vingi ambavyo haviwezi kumvusha.
“Hapa mmehitimu mafunzo yenu ya awali kwa mujibu wa mkataba wenu sasa mtaendelea na mafunzo ya stadi za kazi na ujuzi mbalimbali usiende kujaribu kila kitu chagua kimoja kitakachokufanya uwe hodari kitakachokutambulisha katika maisha yako” amesema.
Nickson amesema kuwa iwapo kijana atajikita kupata ujuzi kwenye eneo moja na kuwa hodari huko ikimsaidia kujiajiri na kuinuka kiuchumi huku akizingatia mafunzo aliyopewa.
Awali mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ambaye ni Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita wa Jeshi la Wanamchi wa Tanzania Meja Jenerali Ibrahim Mhona amewakumbusha vijana hao kuzingatia maamuzi ya kujiunga na Jeshi hilo na kujiepusha na vitendo vya afya ya mwili.
Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanal Robert Kessy alisema lengo la mafunzo hayo kwa vijana ni kukuza mwili wa kizalendo na kuwafanya wajitambue kuwa ni sehemu ya Jamii na kwamba kupitia mafunzo hayo yatawafanya kulitumikia Taifa popote
Kadhalika amesema vijana hao ni vema wakaedeleza waliyojifunza kwenye makambi ambayo watapangiwa wanapokwenda kuanza mafunzo ya stadi za maisha na kujipatia ujuzi ambao utawasaidia kujiajiri.
Mkuu wa Kikosi 832 cha Ruvu( JKT ) Kanali Peter Mnyani alieleza kwamba vijana hao wamefanya mafunzo hayo kwa muda wa miezi minne kati ya 24 kwa mujibu wa mkataba na wamekidhi vigezo vilivyotakiwa na miezi 20 iliyobaki wataendelea na hatua nyingine.
Wakati huo huo Kikosi 832 Ruvu JKT wameanzisha bustani ya wanyama kwa ajili ya kutangaza utalii wa ndani, utalii wa picha na kuhifadhia mazingira.
Afisa Uhifadhi wa Ruvu JKT Ezekiel Molel amesema katika bustani hiyo imeanza na wanyama 17 katika eneo lenye ekari 70 na matarajio ya baadae ni kuwa na shamba kubwa la uhifadhi lenye wanyama wengi watakaovutia kwenye utalii.
Molel amesema wanyama walioanza nao ni wapole ambao ni pamoja na mbinu, swala, pundamilia na nyumbu na kwamba idadi itaendelea kuongezeka kuwarahisiahia wananchi na watalii wengine kutembelea hifadhi hiyo na kuona wanyama sambamba na kupiga nao