Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limekuwa likitoa huduma ya mtandao wa T-Fiber, ikiwa ni pamoja na huduma ya Fiber na Nano (Wireless Fiber), kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa intaneti nchini.
Hata hivyo, kumekuwa na baadhi ya shida zinazowakabili watumiaji wa mtandao wa TTCL, ambao Ulikuwa ukikosa nguvu au kutopatikana kwa siku nzima.
Wateja wamelalamikia hasa kuhusu kasi ndogo ya mtandao wa T-Fiber, licha ya Fiber kuwa na kasi nzuri kutokana na teknolojia yake.
Mmoja wa watumiaji wa mtandao huo ameeleza kuwa wakati mwingine inapotokea shida kwenye mtandao wa Fiber, inaweza kuchukua hadi saa 12 bila kuwa na huduma ya intaneti.
Soma Zaidi:New Report ranks TTCL last in service quality among Tz Networks
Salma Jabir,Mfanyakazi Wa Kampuni ya Usafirishaji iliyopo Posta Dar es Salaam Amesema Kukatika Katika kwa Mtandao Kumepelekea Kutofanya Kazi Zake kwa Muda unaotakiwa ,Huku akiilaumu Kampuni Hio ya Mawasiliano kuwa Sababu Kuu ya Changamoto hiyo.
“Ninakuwa na Kazi nyingi za Kufanya Kupitia Mtandao lakini TTCL wananiangusha sana, Inanifanya niende Na kasi ya Pole pole kutokana na Mtandao Ulivyo, Hali hii inanifanya Kumaliza Kazi Zangu usiku Mno” Alisema Salma.
John Alex, mfanyabiashara wa nguo kutoka soko kuu la Kariakoo, amesema kwamba kukwama kwa mtandao kumemzuia kushirikiana na wateja ambao hununua bidhaa zake mtandaoni, hivyo kusababisha bidhaa hizo kutopatikana haraka na kusababisha athari kwa biashara yake.
“Dunia ipo Kwenye kiganja, Watu wanaagiza Dukani kupitia mtandaoni ambapo tunatangaza biashara, na Mimi ninatumia Simu yenye Mtandao kuwasiliana nao.
TTCL inasumbua mno, na tunatumia kwasababu ya unafuu wa vifurushi vyake lakini kuna wakati unakuwa na kasi ndogo sana.
“Tulijaribu kuwasiliana nao wanasema wanafanya marekebisho lakini hali imekuwa ikijirudia mara kwa mara” John Alex
Akizungumza na Media Wire Express, msemaji wa TTCL amesema kwamba hawajapokea malalamiko yoyote ya changamoto ya mtandao baada ya kufanya maboresho kati ya tarehe 26 hadi 28 mwezi wa 4 mwaka huu.
Pia, amesisitiza kuwa wanafuatilia changamoto za mtandao katika maeneo yanayosumbua na wanajitahidi kuzipatia ufumbuzi kwa haraka.
Ameongeza kwamba mteja yeyote akipata changamoto ya mtandao anatakiwa atoe taarifa kwa watoa huduma ili tatizo lake litatuliwe kwa wakati.
Kwa upande mwingine, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imechapisha takwimu za robo mwaka kuhusu huduma za pesa za simu zinazotolewa na Watoa Huduma wa Mtandao wa Mkononi, ikionyesha ongezeko kutoka akaunti milioni 52.9 kwenye robo inayomalizika Desemba 2023 hadi milioni 53.0 mwezi Machi 2024.
Huku TTCL ikiwa na 2% ya watumiaji wa huduma ya kutoa fedha kupitia mtandao huo.