Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa, kidini na kikabila washiriki kikamilifu kutoa maoni ili kuhakikisha Dira mpya ya Taifa ya Maendeleo inakuwa jumuishi na shirikishi.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa sekta binafsi asasi za kiraia, makundi maalum kama vile vijana, wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na mashirikisho mengine yashirikiane na Tume ya Mipango katika uratibu wa ukusanyaji wa maoni ya wanachama na wadau wao. ”Hii itasaidia kuhakikisha kuwa maoni ya makundi husika yanapokelewa na kujumuishwa katika maandalizi ya Dira mpya ya Taifa ya Maendeleo.”
Waziri Mkuu amesema kazi zinazofuata katika maandalizi ya Dira mpya ya Taifa ya Maendeleo ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kupitia kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji wananchi kushiriki katika maandalizi ya Dira mpya na kukamilisha na kusambaza taarifa ya ukusanyaji maoni.
Would love to forever get updated great web blog! .
Thank you a bunch for sharing this with all folks you actually understand what you are talking about! Bookmarked. Please also consult with my web site =). We may have a hyperlink alternate arrangement among us!