Dark
Light

Matumizi Ya Ardhi Yazingatiwe Yasibadilishwe Bila Kibali- Silaa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ametoa maelekezo matatu kuhusu mipango miji ambapo amesema kuanzia sasa ni marufuku kubadili matumizi ya eneo kwa kutumia vitambaa vya mabango na badala yake ni lazima uitwe mkutano wa wananchi wa mtaa mzima.
March 24, 2024
by

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ametoa maelekezo matatu kuhusu mipango miji ambapo amesema kuanzia sasa ni marufuku kubadili matumizi ya eneo kwa kutumia vitambaa vya mabango na badala yake ni lazima uitwe mkutano wa wananchi wa mtaa mzima.

Waziri Silaa amesema hayo wakati alipofanya ziara katika maeneo ya Oysterbay na Msasani jijini Dar es salaam akiongozana na viongozi wakuu wa Wizara mbapo alikuta baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wameanza kujenga vyumba vya kupangisha vya bishara kinyume na matumizi ambayo ni makazi.

Pili, Waziri silaa amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuunda Kamati Maalumu itakayopitia kiwanja kwa kiwanja ili kubaini viwanja vilivyobadilishwa matumizi na kuvifanyia marekebisho pamoja na kuwaelimisha wananchi wa mitaa hiyo namna bora ya kubadili matumizi.

Maelekezo ya tatu ya Waziri Silaa ni kwa Watanzania wote ambao wanataka kubadili maeneo yao ya makazi kuwa ya biashara basi wawe waungwana kwa kuweka nafasi ya kutosha kwa ajili ya wateja, wapita njia na wananchi wa mtaa huo kupita bila kubabaika.

Waziri Silaa amesisitiza kuwa maeneo ya Oysterbay, Masaki na Msasani ni maeneo nyeti ya makazi yanayobeba taswira njema kwa wawekezaji na wageni kutoka nje, hivyo si vyema kuyafanya yenye vibanda vya biashara badala ya makazi.

 

Cc: Wizara ya Ardhi

2 Comments

  1. I’ve been surfing on-line greater than three hours as of late, but I by no means discovered any attention-grabbing article like yours. It is beautiful value enough for me. In my view, if all webmasters and bloggers made just right content material as you did, the web might be a lot more useful than ever before.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Veep Urges Private Sector for Clean Energy Drive

Vice President Dr. Philip Mpango has called on the private

Tundu Lissu To Appear In Person As Court Rejects Virtual Trial

The Kisutu Resident Magistrate’s Court has ruled that opposition leader