Serikali ya Tanzania na Ujerumani wamekutana na kufanya majadiliano ya ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Serikali hizo mbili yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina Ndogo leo 19 Februari 2024 Dar es Salaam
Aidha katika majadiliano hayo Serikali ya Ujerumani imewasilisha makadirio ya bajeti ya msaada utakaotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini katika Sekta za Maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria.
Majadiliano hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango – Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje – Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani ambaye ameongoza ujumbe wa nchi hiyo, Bw. Marcus von Essen, pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka nchi hizo mbili.
Hiyo ikiwa ni moja ya mijadala ambayo ilianza tangu jumatatu kupitia wizara ya fedha ikiwa ni mikakati ya kuwezesha Tanzania kupiga hatua za kiuchumi wa juu zaidi.