Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema Hati miliki za Ardhi zinazotolewa kwa wamiliki wa ardhi nchini hazitakiwi kuwekewa ‘’Lamination’’.
Mhandisi Sanga ametoa kauli hiyo tarehe 18 Machi 2024 wilayani Chalinze mkoa wa Pwani wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii kukagua utekelezaji Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) katika eneo la Msolwa .
Amebainisha kuwa, wizara yake ya ardhi itaendelea kutoa elimu juu ya suala hilo sambamba na kutoa maagizo kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi kuweka matangazo kwenye ofisi zao kuhakikisha wananchi wanapata elimu kwamba hati milki ya ardhi haitakiwi kufanyiwa ‘’lamination’’ iwe mpya au ya zamani ili kumsaidia mwananchi mwenye hati kufanya muamala anaotaka kufanya.
Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii imehitimisha kutembelea na kukagua miradi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi tarehe 18 Machi 2024 ambapo katika ziara zake imeweza kukagua mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam pamoja na mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi katika eneo la Msolwa lililopo Halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani.
I used to be very pleased to search out this internet-site.I wished to thanks for your time for this glorious read!! I definitely enjoying each little bit of it and I’ve you bookmarked to take a look at new stuff you blog post.