MTV na BET ambao ni wadhamini/media partner wamechagua vipengele sita ambavyo washindi wake watapelekwa kwenda kuhudhuria BET Awards nchini Marekani zitakazofanyika June 30.
Hayo yamesemwa na Seven Mosha, Makamu Mwenyekiti Wa TMA 2024 Kwenye Mkutano na waandishi Wa Habari Juma Hili.Tuzo za TMA mwaka huu zitaonekana kwenye vituo vya runinga vya MTV na BET.
“Wataweza kuhudhuria tuzo, pre party, post party na wataweza kujumuika na wasanii wa Afrika pia ambao wanaweza kuwa nominated kwenye the music awards. Na kwenye pre party pia kutakuwa na different performances ambapo pia wasanii hawa wataweza kutumbuiza vilevile,” Ameongezea Seven Mosha
Pia, vimealikwa vyombo vya habari vya kimataifa kufanya coverage ya tuzo hizo ambavyo ni pamoja na Billboard, Okay Africa, Variety na Rollingstone Africa.
Tuzo za mwaka huu zitakuwa na event mbili, TMA Prelude itakayofanyika June 14 ambapo kutatolewa tuzo 20 za mwanzo.
June 15 ni TMA Red Carpet, Main Event & After Party na jumla ya tuzo 17 zitatolewa.
Kuanzia May 5 hadi 9 wasanii watapaswa kuwasilisha kazi zao ambazo zimetoka kuanzia January 1 hadi December 30, 2023. Screening itafanyika kuanzia May 10 hadi 11 na kufuatiwa na tathmini ya academy May 12.
Upigaji kura utafanyika May 13 hadi June 11.