Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi ya kurejea nauli za mabasi yanayotoa huduma ya usafiri wa haraka kutoka kwa UDART ambayo inatoa huduma za mpito za usafiri wa Mabasi ya Haraka katika Jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo:
1. Nauli kwa Abiria Njia Kuu (Truck Route) = 1,000TZS
2. Nauli kwa Abiria Njia Lishi (Feeder Route) = 600TZS
3. Nauli kwa Abiria Kimara – Kibaha 1,200TZS
4. Nauli kwa Mwanafunzi = 200TZS
Kwa mujibu wa Kifungu cha 21 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka inapaswa kupokea maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwemo nauli za mabasi. Katika kulitekeleza hilo, Mamlaka imeandaa mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa usafirishaji, ikiwa ni pamoja na watoa huduma, watumiaji wa huduma na wananchi kwa ujumla.
Soma:DART Imewsimamisha Kazi Madereva Waliopeleka Abiria Morocco Badala Ya Kimara
Mkutano huo utafanyika tarehe 03 Julai 2024 katika Ukumbi wa mikutano Arnaoutouglou, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3.30 asubuhi. Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, LATRA inawaalika wadau wa sekta ya barabara na wananchi kwa ujumla kushiriki bila kukosa katika mkutano huo muhimu.
Kwa watakaoshindwa kufika kwenye mkutano huo, wawasilishe maoni yao ya maandishi katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu iliyopo katika Jengo la Mkandarasi, Tambukareli Dodoma na Ofisi za Mikoa za LATRA kabla ya tarehe 19 Julai, 2024. Aidha, maoni ya wadau yanaweza kutumwa kwa barua pepe kupitia anuani zifuatazo: info@latra.go.tz na dg@latra.go.tz
Some really nice stuff on this internet site, I enjoy it.
This is very interesting, You are a very skilled blogger. I’ve joined your rss feed and look forward to seeking more of your fantastic post. Also, I have shared your web site in my social networks!
Respect to author, some fantastic information .