Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka kwenye ukurasa wake wa instagram ikimuonesha amepaka “bleach” ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa Wachezaji na wafuasi wa Yanga Sc kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad utakaopigwa Jumamosi katika dimba la Benjamin Mkapa.
Mchezo huo umepewa jina la Pacome Day ambapo washabiki wa timu hiyo wameelezwa kuwa wanaweza kupaka rangi nywele zao za kichwani, ndevu ili kuendana na siku hiyo