Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka watu wanaotumia fedha kuwatuma watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan mtandaoni kuacha mara moja na endapo wataendelea, Jumatatu ya Aprili 15,2024 atawajata.
Makonda amesema, “Wapo watu wanaotumia fedha kuwaagiza watu kumtukana Rais Samia, naomba waache mara moja, ninawafahamu kwa majina, msipoacha Jumatatu nitawataja, wapo hadi mawaziri.”
Makonda amesema hayo leo Aprili 12, 2024 kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine yaliyofanyika Monduli mkoani Arusha.
Read: Makonda hints Possibility of Monthly Public Audience with Samia
https://mediawireexpress.co.tz/makonda-hints-possibility-of-monthly-public-audience-with-samia/
“Ni jambo la kusikitisha kwa baadhi ya viongozi kutotambua dhamana walizonazo…badala ya kuleta utulivu na maelewano kati ya serikali na jamii, wanatumia nafasi zao kuleta uchonganishi kati ya jamii na serikali…” – Rais Samia Suluhu Hassan akiwasihi viongozi walioteuliwa kutumia dhamana za nafasi walizopewa kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao.
Rais Samia ametoa pole kwa wananchi wate waliopatwa na athari za mafuriko pamoja na ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya msingi Ghati Memorial ya jijini Arusha iliyotokea leo baada ya kusombwa na maji katika eneo la Engosengiu kutokana na uzembe wa dereva na kusababisha vifo vya wanafunzi watano.
Read: Makonda Umechangamsha Chama ,Nakuamini-Rais Samia
https://mediawireexpress.co.tz/makonda-umechangamsha-chama-nakuamini-rais-samia/
Amewataka pia wananchi kuchukua tahadhari juu ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.