Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume hajaridhishwa na tabia ya baadhi ya Waandisi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuandaliwa na kufanyiwa makisio ya gharama za michoro na mkandarasi.
Dkt. Mfaume ameyasema hayo leo Februari 26,2024 alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Arusha
Amesema makadirio hayo huwa yanafanywa na Mhandisi wa Halmashauri hivyo mkandarasi hapaswi kuandaa baada ya kukabidhiwa kazi kwa kuwa inaongeza gharama za mradi na kuitia hasara Serikali.
” inasikitisha kazi ambayo inatakiwa kufanywa na mhandisi inafanywa na mkandarasi, hili halikubaliki ni kosa kisheria.” Amesema Dkt. Mfaume.
Hata hivyo Dkt. Mfaume amesikitishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa jengo hilo ambalo lilitengewa fedha mwaka 2022/2023 lakini mpaka leo lipo katika hatua ya msingi.
Aidha, amezitaka Timu za usimamizi na uratibu wa shughuli za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii ngazi ya Halmashauri (CHMT) na Mkoa (RHMT) kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mara kwa mara ili kuhakikisha.
Sambamba na hilo ameeleza kuwa Kituo cha afya Levolosi kimepokea shilingi milioni 642 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 500 ni fedha toka Serikali kuu na shilingi milioni 142 ni fedha za mapato ya ndani