Daktari Wa Magonjwa ya Akili Kutoka Hospitali Ya Rufaa,Mkoa Mwananyamala, Dkt Jovina Josephat amesema moja ya viashiria vya Mtu Kusumbuliwa na Ugonjwa Wa Akili ni Wivu Ulio Pitiliza Ambao Umekuwa Changamoto Kubwa Hasa Kwa Watu Waliopo Kwenye Mahusiano au Wanandoa.
Dkt. Jovina amesema Afya Ya Akili Imekua Ni Changamoto Kwa Watu Wengi Duniani, Huku Wengi Wakiishi Na tatizo Hilo Kwa Kutokujua , Ugonjwa Huu Umekuwa Na Visababishi Kadha Wa Kadha Huku Madhara Yake Yakiwa Makubwa,Kama Kujinyonga, Kufanya Ukatili Wa Kijinsia Hata Kufanya Mambo Yanayoashiria Upungufu wa Akili.
Pia Dkt Jovina Ameeleza kwamba Ugonjwa Wa Akili ni tatizo la Ubongo Ambao humuathiri Mtu Kifikra,Kihisia Na Kimatendo Tofauti Ambayo ni Tofauti Ya Yaliyotarajiwa Kijamii.
“Tunachangamoto ya Afya Ya Akili Na Tunamaradhi Ya Afya ya Akili Ambayo Hubebwa na Dalili Ambazo Huthibitisha Kuwa Mtu Huyu Ana Afya Ya Akili” Amesema Dkt, Jovina
Daktari Amesema ,Moja ya viashiria vya Mtu Kusumbuliwa na Ugonjwa Wa Akili ni Wivu Ulio Pitiliza Ambao Umekuwa Changamoto Kubwa Hasa Kwa Watu Waliopo Kwenye Mahusiano Pamoja Na Wanandoa.
Read more: Call for Government Action on Mental Health and Productivity
https://mediawireexpress.co.tz/call-for-government-action-on-mental-health-and-productivity/
Kiukweli Watu Wamekuwa Wakifanya Matukio Mengi Yakutisha Kama Kuwauwa Wapenzi Wao Kikatili Na Kwa Unyama Makubwa Sababu Tu Ni Wivu Wa Kupindukia, Yaani Mtu Anahisi Tu Anasalitiwa Bila Hata Ya Ushahidi Wakutosha, Huo Ni Ugonjwa Wa Akili Na Mtu Huyu Anahitaji Matibabu Ya Haraka” Amesema Daktari JovinaJovina
Pia Ameongeza Kuwa Njia Pekee ya Kuwasaidia Watu Walioathirika Na Ugonjwa Huu ni Ushauri Wakumwona Mtaalamu wa Afya ili Kuweza Kuepusha Maaafa Makubwa Kama Mauaji Yakinyama Na Mwishoe Kuishia Jela.
Jovina Amesema Hospitali ya Rufaa Mkoa Mwananyamala Inapokea Takribani Wagonjwa 50 Hadi 60 Kwa Siku, Tofauti na Miaka Mitatu Nyuma Ambapo Hospitali Ilikuwa Ikipokea Takribani Wagonjwa 8 Hadi 15 Kwa Siku.
“Hii inaonesha Changamoto Hii imekua Kubwa Sana Nchini na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Kazi,Mapenzi Na Hata Utumiaji Wa Madawa Ya Kulevya Nj Sababu Kubwa Za Ongezeko Kubwa La Idadi Ya Watu Wasumbyuliwao na Ugonjwa Wa Akili Tanzania” Amesema Daktari Jovina.
Créez votre profil dès maintenant et lancez-vous !