Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watu tisa (9) wakituhumiwa kuhusika na tukio la mauaji ya mtoto Asimwe Novart mwenye umri wa miaka miwili na nusu mwenye ualbino ambaye aliporwa na watu wasiofahamika kutoka kwa mama yake mzazi Mei 30, 2024 katika kijiji cha Bulamula Wilaya ya Muleba mkoani Kagera na Mwili wake kupatikana Juni 17, 2024 Ukiwa hauna baadhi ya Viungo katika kijiji cha Makongora.
Taarifa iliyotolewa Msemaji wa jeshi la Polisi DCP David Misime imeeleza kuwa Baada ya tukio hilo kutokea Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama kama hivyo walianza msako mkali kuanzia Mei 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia Juni 19, 2024 ambapo watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya mtoto Asimwe Novart wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta mteja.
Watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu. Pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.
Soma zaidi: Kifo Cha Mtoto Mwenye Ualbino Chazua Taharuki
Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.
Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo.
“Watu waache kudanganyana kwamba kuna utajiri unaopatikana kwa kumiliki viungo vya binadamu mwenye ualbino kwani si kweli kwasababu kama ingekuwa hivyo familia zenye watoto au ndugu wenye ualbino wangekuwa na utajiri mkubwa lakini badala yake tunaona wakiishi maisha ya kawaida kama sisi wengine.” – Msemaji wa jeshi la polisi, David Misime
You can also visit to speak to a counsellor online.
I’m so happy that this sequence is over and that I will never choose up any of these books from this series again for as long as I stay.
I’m the definition of accomplished. Also, spoilers will
likely be abound and aplenty throughout this complete
overview, and this is going to a a largely Supernatural
gif-filled extravaganza, as a result of A). That’s how angels/demons/and many
others. must be finished and B). I can. So if you do not
like spoilers or Supernatural, depart now, as a result of shit’s
about to get