“Kuhusu suala la mimi (Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa) kuwa Mbunge tangu mwaka 2005 na hivyo ni mzoefu na ninafahamu ipasavyo sheria, kanuni na taratibu zinazoliongoza Bunge, nipende kumjibu Mheshimiwa Spika (Dkt. Tulia Ackson) kuwa ni kweli kabisa mimi Luhaga Joelson Mpina, Mbunge wa jimbo la Kisesa (CCM) tangu mwaka 2005 (miaka 19 sasa) mara zote nimekuwa mzingativu wa sheria, kanuni na taratibu zinazoliongoza Bunge, mfano Mei 03.2023 na Juni 04.2024
Mheshimiwa Spika (Dkt. Tulia Ackson) aliniagiza kuleta ushahidi nikatii tena kwa wakati uliopangwa, agizo la kuitikia wito wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge nilitekeleza tena kwa wakati, maamuzi ya kuhamishwa kamati ya Bunge kabla hata ya kipindi cha kubadilishiwa kamati niliyapokea na kutekeleza (mimi nilikuwa Mjumbe wa Kamati ya Bajeti hapo katikati mwaka 2022 ghafla nikaleletewa taarifa kwenye kamati kuwa natakiwa nihame muda huohuo nihamie kamati nyingine, na nikabebewa mpaka na vifaa), utaratibu wa kubadilishwa kamati huwa Wabunge wakipangiwa kwenye kamati wanaitumikia nusu kipindi (kwa maana ya miaka ya miaka miwili na nusu, yaani nusu ya miaka mitano) lakini nilikuwa nimetumikia kamati hiyo kwa mwaka mmoja tu nikaletewa uhamisho tena wa haraka (msaidizi wa Bunge alinipigia Simu anasema Mheshimiwa Mpina tunakuja hapo tunakuletea Barua Mheshimiwa Spika ameamua kukuhamisha kamati na unatakiwa kuhama mara moja na tutakuja kukusaidia kubeba mizigo)” -Mpina
Soma Zaidi:Mpina Afungiwa Vikao 15 Bungeni
“Ilikuwa kama vile nafukuzwa, kama vile kuna jambo lililotakiwa kufanyika kwenye Kamati ya Bajeti na mimi sikutakiwa kuwepo, nikahamishwa kama mwizi kwenye hiyo kamati lakini sikuwahi kulalamika mahala popote wala hata kuzungumza na vyombo vya habari bali nilivumilia tu kwa sababu mimi siwezi kushindwa kufanya kazi na kamati yoyote, nimeenda Kamati ya Katiba na Sheria nikaendelea kufanya kazi vizuri tu, wala sikulalamika hata kwake (Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson) sikwenda kumwambia kwanini umenitoa kwenye Kamati ya Bajeti, na kwakweli mimi nimekaa kwenye kamati za fedha muda wote lakini nilikubaiina wala sikulalamika” -Mpina Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina amezungumza hayo alipokutana na wanahabari Juni 29.2024
I truly enjoy examining on this site, it contains great posts. “One should die proudly when it is no longer possible to live proudly.” by Friedrich Wilhelm Nietzsche.