Dereva wa gari la mizigo Adriano Samweli (40) mwenyeji wa Kigoma, amefariki dunia katika ajali iliyotokea Kijiji cha Igumbilo, Kata ya Lupila wilayani Makete mkoani Njombe baada ya kushindwa kulimudu gari hilo na kisha kutumbukia korongoni.
Ajali hiyo imetokea usiku kuamkia jana Juni 8, 2024 katika Mtaa wa Ihagala, Kitongoji cha Kisekelewe ambapo gari hilo lilibeba viazi na kulikuwa na watu wanne.
Utingo wa gari hilo, Riziki Shaban ameeleza namna alivyonusurika katika ajali hiyo kwa kusema ni kwa neema za Mungu kwani lilipoanza kubiringika yeye lilimtupa nje na kuendelea kuporomokea korongoni.
Soma:Dereva Shabiby Atuhumiwa Kusababisha Ajali majeruhi 22
Mashuhuda wameeleza namna walivyoshirikiana kuwaokoa watu waliokuwemo kwenye gari hilo baada ya ajali kutokea, na kulazimika kuchimba shimo ili kuweza kuutoa mwili wa marehemu.
Mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya Lupila, Dk Isack Lulindi akizungumza ofisini kwake amesema ni kweli walipokea majeruhi watatu ambao wamewatibu na tayari wameruhusiwa, pia wamepokea mwili wa mtu mmoja akiwa amefariki dunia na umehifadhiwa kituoni hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akitaja kuwa chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari hilo na kutumbukia korongoni.
Kamanda Banga ametoa wito kwa madereva wageni na jiografia ya Mkoa wa Njombe kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuwatumia wenyeji wanapokuja kuchukua mizigo ili kuepusha matukio ya ajali.
Source: Mwanachi Digital
Great – I should certainly pronounce, impressed with your site. I had no trouble navigating through all the tabs and related info ended up being truly simple to do to access. I recently found what I hoped for before you know it in the least. Quite unusual. Is likely to appreciate it for those who add forums or anything, site theme . a tones way for your client to communicate. Excellent task..