Wahenga walitangulia Kusema, Apigae Mbija Mwishoe Huimba, Naukiona Mawingu Yametanda Angani, Basi Inakaribia Kunyesha.
Wahenga Si wendawazimu Kuyasema Haya, Nayathibitisha Kwa ukakamavu Nikiifikiria Kesho (20/04/2024) , Siku ya Derby ya Kariakoo , Mechi Iwakutanishayo Wanasimba Na Yanga Katika Dimba la Benjamin Mkapa ,Kuupiga Mtanange wa Mzunguko Wa Pili Katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara
Soma:
Media Wire Express ,Imepita Kona Kwa Kona Katika Viunga Mbali Mbali Vya Jiji La Dar Es Salaam Kutega Sikio za Tambo Za Mashabiki Wa Timu Hizi Mbili Kongwe Hapa Nchini,
Lakini Kilichoshangaza Maskio Yangu Ni Kuona Baadhi ya Mashabiki Kutoka Pande Zote Mbili Wakihusisha Kunyesha Kwa Mvua Nyingi Kama Ishara Njema Ya Kumfunga Mtani wake.
Salma Rajabu Mshabiki Wa Simba Kutoka Soko Kuu La Kariakoo, Amejinasib Timu Yake Kushinda Katika Mtanange Wa Kesho Dhidi Ya Young Africans Kutokana Na Kuwa na Matokeo MazuriHasa Pale Wanapokutana Wakati Wa Mvua.
More On ; Rekodi zaibeba Simba kwa Yanga
https://www.mwananchi.co.tz/mw/michezo/rekodi-zaibeba-simba-kwa-yanga-4201134
“Kiukweli, Mi nasemaje, Kesho Kitaumana, Na Mvua Hii, Lazima Simba Ashinde, Sababu Tumemkanda Sana Mtani Wakati Mvua, Kama Huamini, Nikukumbushe mechi ile Ya Kibu Denis na Inonga Varane, Tuliwakanda Mbili hadi Kibu Aka Slide(Kuteleza) Kama Drogba, Kwahio Kesho Ukiona Imenyesha , Mwananchi Ninae” Amesema Halima ,Shabiki Wa Simba.
Alipo Zinduna Basi Zinduna Haipo Mbali, Ni Msemo Adhimu Wa Wahenga Unaonikumbusha Yakuwa ,Alipo Simba Basi Young Africans Hakosi, Shija Athman Kutoka Soko Kuu la Kariakoo, Akajinasib Kuwa Kama Shida ni Mvua, Tayari Timu Hiyo Waliwahi Kupata Matokeo Bora Mbele Ya Simba
” Mwandishi Ngoja Nikukumbushe Jambo, Maana Binadamu Tumeumbiwa Kusahau, Unaimumbuka Ile Mechi Ya Simba Na Yanga , Bernard Morrison Akiwa Wamoto Yanga, Aliwafunga Goli La Faulo, Siku Ile Mvua ilikuwa Kali Mnoo, Lakini Chuma kikaingia Na Mechi Ikaisha Moja Bila, Sasa Hawa Wanadahani Mvua ikiwepo wanashinda Wao, Niwaambie Tu Chura Anapenda Maji Lakini si yamoto, Na Raha ya Goli Bao, Kesho hawatoamini macho Yao.” Alisema Shija Athman, Shabiki wa Young Africans.
Ikumbukwe Mamlaka Ya Hali ya Hewa TMA imethibitisha kuwepo Kwa Mvua Kesho Tarehe 20/ 04/2024. Katika Jiji La Dar Es Salaaam, Siku Ambayo Itawakutanisha Wapinzani Wawili Katika Mpira wa Tanzania ,Simba Na Yanga, Majira ya SAA 11 Jioni Pale Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Nani Atatamba Na Kuibuka Na Matokeo Mazuri kesho Licha ya Uwepo Wa Mvua, Ni Swala la Muda Tu.