Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya ya rejareja kwa lita ya petroli kufikia Sh3,314 ikiwa ni bei ya juu zaidi tangu Sh3,410 iliyotangazwa Agosti, 2022.
Bei ya petroli kupitia katika bandari ya Dar es Salaam inayoanza kutumia Mei 01, 2023 ni ya juu zaidi katika kipindi cha miezi 20 iliyopita.
#BEI:EWURA imetangaza Bei za Bidhaa za Petroli Kuanzia tarehe 1 Mei 2024; saa 6:01 usiku.
✓https://t.co/w3a4VMVRc1#beizamafuta #petroli #beikikomo #EWURA pic.twitter.com/k8qeZZ6uBz— EWURA Tanzania (@EwuraTanzania) May 1, 2024
Katika kipindi hicho hakukua na bei ya juu iliyozidi hiyo wakati iliyokaribia ni Sh3,281 ya Oktoba 2023. Vilevile bei ya chini zaidi ilikua Sh2,736 ya Julai 2023.
Bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3314 kwa lita, dizeli Tsh. 3196 na mafuta ya taa 2840.
Soma zaidi: Bei Ya Petrol Yaongezeka Lita Tsh. 3257 EWURA Yatangaza
Kwa mujibu wa Ewura, mabadiliko ya bei za mafuta kwa Mei 2024 yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 3.90 kwa mafuta ya petroli na kupungua kwa wastani wa asilimia 1.31 kwa mafuta ya dizeli.
Wakati bei ya petroli ikipanda bei ya dizeli imeendelea kushuka na kufikia Sh3,196 kwa Mei mwaka huu ikiwa ni Sh252 pungufu ukilinganisha na miezi saba iliyopita.
Vilevile bei ya Sh2,840 ya lita ya mafuta ya taa iliyosalia kwa miezi minne mfululizo ni chini zaidi katika miezi 21 iliyopita, ambapo Agosti 2022 ilikua Sh3,765 ambayo haijawahi kufikiwa.