Mtu mwingine ametoa madai mapya ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya tajiri wa muziki, Sean “Diddy” Combs. April Lampros, aliyekuwa mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Mitindo, amefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Kaunti ya New York, akidai kuwa Diddy alimnyanyasa kingono mara kadhaa katika miaka ya 1990 baada ya kumuona katika baa moja huko SoHo mwaka 1995.
Lampros anasema kuwa Diddy alimzawadia zawadi na maua kabla ya kumsongeza kwenye hoteli na kumdhalilisha kimwili. Aidha, anadai kuwa Diddy alimwahidi msaada katika sekta ya mitindo ikiwa atajitolea kufanya mapenzi naye.
Soma Zaidi:Diddy Hadharani Baada ya Kuomba Msamaha kwa Cassie!
Hii ni kesi ya pili wiki hii dhidi ya Combs, baada ya Crystal McKinney kumshtaki kwa unyanyasaji aliopata katika studio yake ya kurekodi muziki mwaka 1999 ambapo McKinney alikuwa na umri wa 22 na Combs akiwa na 34. McKinney pia anadai kuwa Combs alimzuia kuingia kwenye tasnia ya mitindo.
Madai haya mapya yametokea miezi michache tu baada ya matukio ya kufwatilia kesi ya Diddy kuhusu unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamke mwingine katika miaka ya 1990. Ingawa mashtaka hayo yalitupiliwa mbali, madai haya mapya yanaweza kuwa na athari kubwa kwa sifa na biashara za Combs.
Waakilishi wa Combs bado hawajatoa maoni rasmi kuhusu madai haya mapya. Hata hivyo, kuna wasiwasi kuwa matukio haya yanaweza kuwa na athari kubwa kiuchumi na kijamii kwa nyota huyu maarufu wa muziki na filamu.