Klabu ya Young Africans Imefungua Tawi Lake Huko Nchini Pretoria Nchini Afrika Ya Kusini; Nia ikiwa kutanua Zaidi Nembo ya Klabu hio na Kuwaunganisha Mashabiki wake Waliomo Nchini Humo.
Akiongea na Wanachama ,Viongozi Pamoja Na Wanahabari, Rais wa Timu hiyo Amesema Timu yao Inamatawi Lukuki Katika Nchi Mbali Mbali ikiwemo Marekani
“Niweke Rekodi Sawa, Sisi tuna Matawi Lukuki Nje ya Mipaka Ya Tanzania, Kwa mfano kule Marekani Tunalo tawi la Uanachama” Amesema Eng.Hersi
“Niwapongeze sana idara ya habari na Wanachama kwa kuweka mipango mikakati madhubuti ya kampeni ya “Twenzetu kwa Madiba”. Ama kwa hakika idara hizi mbili zina watu wenye upeo mkubwa wa maarifa wa kuanzisha agenda zenye dhima kwa Klabu”
“Nichukue nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana mashabiki wa Young Africans SC hapa Afrika Kusini” Eng. Hersi
Read>> http://Mamadou Gaye Awaonya Mamelodi Dhidi Ya Yanga
“Klabu ya Young Africans SC inaendelea kuweka rekodi ya kuzindua matawi nje ya mipaka ya Tanzania. Tumefungua tawi kule nchini DR Congo, na leo tumezindua tawi lingine hapa nchini Afrika Kusini. Tunaposema sisi ni wakubwa tunamaanisha” Ibrahim Samwel – Mkurugenzi wa Masoko, Wanachama na Mashabiki Young Africans SC
“Wale Mashabiki wetu waliosafiri kwa njia ya Basi tayari wameshaingia nchini ya Afrika Kusini. Tunaomba Mashabiki wa hapa Afrika Kusini kujumuika na hawa wenzetu waliotoka Tanzania kwenda kutafuta matokeo hapo kesho” Ali Kamwe
Read>> https://mediawireexpress.co.tz/president-doubles-goal-motivation-package-for-simba-young-africans/
“Hii ni ndoto ambayo tumeisubiria kwa muda mrefu sana. Tunamshukuru sana Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Said kwa kuitikia wito wetu wa kuzindua tawi hili. Tunasisitiza mashabiki wengine ambao wapo hapa Afrika Kusini wajitokeze kwa wingi” Emson Mchau Katibu wa tawi jipya la Young Africans – Afrika Kusini.
Ikumbukwe Timu ya Yanga Kesho Itakuwa na Mchezo wa Mkondo wa Pili Ligi ya Mabingwa Afrika Dhidi ya Mamelodi Sondown ya Huko Afrika Kusini Ikiwa Mechi Ya Awali wakitoka Suluhu ya Bila Kufungana Katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
You made some good points there. I did a search on the issue and found most persons will consent with your website.
Thank you for another wonderful article. Where else may just anyone get that type of info in such a perfect method of writing? I have a presentation subsequent week, and I’m at the search for such info.