Watu Tisa wamefariki Dunia na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiriki kugongana uso Kwa uso na Lori la mizigo, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
Akitoa taarifa hiyo Kwa vyombo vya habari, mjini Kibaha, Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Pius Lutumo,alisema ajali hiyo ilitokea Machi10, 2024, majira ya 11:15 jioni,eneo la Kilomo, wilayani ya Bagamoyo katika barabara kuu ya Bagamoyo Dar es Salam.
Alisema gari lenye nambari za usajili T. 503 DRP lenye tela namba T733DUQ Lori aina ya Howo Malo ha VRK Limited likiendeshwa na Dereva Apolo Isdor Mgomela (52) liligonga uso Kwa uso gari ya abiria aina ya Kosta yenye namba za usajili T. 676 DSM likiendeshwa na dereva Juma Mackey na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
“Watu Tisa wamefariki ikiwemo madereva wa magari yote mawili, gari aina ya Kosta ilikuwa ilitokea Bagamoyo kuelekea Dar es Salam na Lori lilikuwa likitokeana dar Es Salam kwenda Bagamoyo”alisema Kamanda Lutumo.
Aidha alisema chanzo Cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori kuyapita magari mengine pasipo kuchukua tahadhari jambo lililosababisha kwenda kugonga gari ya abiria uso Kwa uso na kusababisha vifo hivyo.
Aidha alisema majeruhi watatu wa ajali hiyo wanendelea kupatiwa matibabu hosiptali ya wilaya ya Bagamoyo huku miwili ya marehemh ikihifafhiwa hosptalini hapo kusubiri taratibu za mazishi.
Kufuatilia ajali hiyo jeshi la polisi mkoa wa Pwani, limetoa wito Kwa wananchi wote watumiaji wa barabara ikiwemo madereva wanatakiwa kufauta na kuzingatia sheria za usalama wa barabarani ili kuondokana na ajali za mara Kwa mara.
Fascinating blog! Is your theme custom made or did you download it from somewhere? A theme like yours with a few simple tweeks would really make my blog jump out. Please let me know where you got your design. Cheers