Rapa maarufu Roddy Ricch amefikia makubaliano na aliyekuwa mpenzi wake, Alexandra Kiser, kuhusu malezi ya mtoto wao mwenye umri wa miaka mitatu. Katika makubaliano hayo, Roddy Ricch amepewa haki ya kumuona mtoto wake mara mbili kwa wiki, Jumanne na Alhamisi.
Mbali na haki hiyo, Roddy Ricch ametakiwa kulipa kiasi cha dola za Kimarekani 8,000, sawa na takribani shilingi milioni 20 za Kitanzania kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto. Fedha hizi zitagharamia mahitaji muhimu kama vile ada za shule, gharama za matibabu, na matumizi mengine muhimu kwa ustawi wa mtoto.
Aidha, rapa huyo pia amekubali kulipa gharama za kuendesha kesi hiyo ambazo zilifikia dola za Kimarekani 37,500, sawa na zaidi ya shilingi milioni 97 za Kitanzania. Gharama hizi zilitumika kufungua na kuendesha shauri hilo na zitalipwa moja kwa moja kwa Alexandra Kiser.
Makubaliano haya yanakuja baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya pande hizo mbili. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na Roddy Ricch, rapa huyo ameonyesha nia ya kuhakikisha kuwa mtoto wake anapata malezi bora na yote anayohitaji kwa ukuaji mzuri.
SomaZaidi;Diddy Hadharani Baada ya Kuomba Msamaha kwa Cassie!
Roddy Ricch, ambaye jina lake halisi ni Rodrick Wayne Moore Jr., amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki na kujizolea umaarufu mkubwa kupitia nyimbo zake kama “The Box” na “High Fashion”. Licha ya mafanikio hayo, rapa huyo sasa anakabiliwa na changamoto ya kusawazisha kati ya majukumu yake ya muziki na majukumu ya kuwa baba.
Kwa upande wa Alexandra Kiser, ameelezea kuridhika na makubaliano hayo na matumaini kuwa yatasaidia kuhakikisha kuwa mtoto wao anapata mazingira bora ya kukua na kuendelezwa.
Makubaliano haya yamehitimisha mgogoro wa kisheria uliokuwa ukimkabili rapa huyo na sasa ameelekeza nguvu zake kwenye kuhakikisha ustawi wa mtoto wao unakuwa kipaumbele.