Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza viongozi na watendaji wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzingatia nidhamu na maadili katika kazi akisema kuwa sehemu pekee iliyobaki na nidhamu ni baadhi ya majeshi kwakuwa wanaogopa kufanya makosa watauwa watu.
Rais Mwinyi akizungumza katika Kongamano la Kiimani kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na kuratibiwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ukumbi wa Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 6 Aprili 2024
Katika hotuba yake, Rais Mwinyi amesisitiza umuhimu wa nidhamu katika utumishi wa umma ,amekumbusha kwamba nidhamu si suala linalohusu majeshi pekee bali linapaswa kuwa msingi katika kila ngazi ya utawala.
“Pale ambapo kuvunjika kwa nidhamu kutaleta maafa , leo katika wakati tuiokuwa nayo sehemu iliyobaki na nidhamu ni katika majeshi tu, na sio majeshi yote. kwasababu ukivunja nidhamu utauwa watu na utachukuliwa sheria kali,utapelekwa kwenye koti masho.kwa bahati mbaya kwenye utumishi wa umma hatuoni kama kuvunja nidhamu kutaleta maafa ndio maana kuna mmomonyoko wa nidhamu na maadili” Rais Mwinyi
Amefafanua kuwa “nidhamu inahitaji kuambatana na maadili, uwajibikaji, mshikamano, na umoja”.
Read>> http://Zanzibar Emphasizes Religious Tolerance
Rais Mwinyi amewataka viongozi kuzingatia uaminifu na kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao, Amesisitiza kuwa uaminifu na kutenda haki ni silaha kubwa katika kukuza maadili na kuleta mabadiliko chanya katika utumishi wa umma.
Aidha, Rais Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kusaidiana na kushirikiana katika kutenda haki na kutimiza majukumu kwa manufaa ya wote. Ameeleza kuwa imani na hofu ya Mungu ni muhimu katika kubadilisha tabia za watu na kuwafanya wawe na hofu ya Mungu.
Kongamano hilo la kiimani limekuwa jukwaa la kipekee ambalo limewawezesha viongozi na watendaji wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu umuhimu wa nidhamu, maadili, uwajibikaji, na umoja katika utumishi wao.
Read>> https://mediawireexpress.co.tz/zanzibar-government-lowers-sugar-as-ramadan-begins/