Dark
Light

Mkoa Wa Dar Es Salaam Upo Salama Hakuna Mauaji-CHALAMILA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkoa huo uko salama na hakuna mauaji yaliyorindima na atahakikisha watakaosababisha mauaji kutokea watachukuliwa hatua.
April 3, 2024
by

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkoa huo uko salama na hakuna mauaji yaliyorindima na atahakikisha watakaosababisha mauaji kutokea watachukuliwa hatua.

Amesema: ‘’Tumetoka kwenye pasaka, kuna gazeti liliandika mauaji yarindima alafu pembeni wakamuweka ndugu yangu Muliro, nikuhakikishie mheshimiwa Rais, hakuna mauaji yaliyorindima Dar na kama yatakuja kurindima basi watakaosababisha yatawakuta makubwa’’
Chalamila amesema hayo leo Aprili 3,2024 aliposhiriki hafla ya uzinduzi wa tume ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Pia amesema kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya wote kutoka Mkoa wa Dar es Salaam. watahakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi Mkuu unaofanyika mwakani kuwa imara

Read>>http://Hakuna Sheria Kuwakamata Wanaokula Mchana-CP Hamad
Read>> http://Polisi Kuimarisha Ulinzi Kuelekea Sherehe Z a Pasaka
“Na nitoe rai Mh Rais mwaka huu tuna uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani tuna uchaguzi mkuu, mara nyingi wawekezaji wanashindwa kuweka mitaji mingi kwenye uwekezaji wa kisekta mbalimbali wakihofia vurugu ambazo huwa zinakiuwepo wakati wa uchaguzi, mwaka huu tunaomba tukuhakikishie, tunashirikiana kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa imara na utakuwa safi na wale wote wenye mataji yenu msiogope kuwekeza” amesema Chalamila

‘’Mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa, sisi viongozi tunathibitisha kwamba uchaguzi utakuwa imara, amani na utulivu itakuwa ndiyo kipaumbele chetu.’’

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Mwanyika Urges Business Community to Support Warehouse System

The Chairman of the Permanent Parliamentary Committee on Industry, Trade,

Four U.S. Soldiers Killed in Lithuania Training Accident

NATO has confirmed that four U.S. soldiers who went missing