Bunge la Tanzania linatarajia kupiga kura ya wazi leo, ambayo itaamua hatma ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25. Zoezi hili la kupiga kura linafuata siku saba za majadiliano juu ya bajeti hiyo, ambayo iliwasilishwa bungeni Dodoma Juni 13 mwaka huu.
Wabunge wataitwa mmoja mmoja kupiga kura ya NDIYO, HAPANA au KUTOKUAMUA. Hii ni bajeti ya nne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mjadala ulikuwa mkali, huku hoja mbalimbali zikiibuka, ikiwemo suala la upungufu wa sukari nchini, uwekaji tozo kwenye gesi ya magari, kikokotoo na hali ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ubadhirifu wa mali za umma, ubovu wa barabara na madeni ya wakandarasi pamoja na ugumu wa upatikanaji wa dola.
SomaZaidi;Deni la Serikali Linafikia Trilioni 91.7
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo watazipatia majibu hoja hizo kabla ya zoezi la upigaji kura kuanza.
Baada ya kupiga kura, kura hizo zitahesabiwa na uamuzi wa bajeti hiyo utatolewa endapo imepitishwa ama la. Ikiwa Bunge litakataa kupitisha bajeti iliyopendekeza na Serikali, Rais atalivunja kwa mujibu wa Katiba.
You actually make it appear so easy together with your presentation however I find this topic to be actually one thing which I believe I’d by no means understand. It sort of feels too complex and extremely extensive for me. I am looking ahead for your next submit, I?¦ll attempt to get the hold of it!