Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Waziri Mkuu Akagua Athari Za Maafa Rufiji

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Ikwiriri, Rufiji akitokea Mlimba, Morogoro aliwaomba wananchi hao waendelee kutulia kwani serikali iko nao na itaendelea kuwahudumia hadi hali yao irejee katika hali ya kawaida.
April 17, 2024
by

Wazri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi waliokumbwa na adha ya mafuriko nchini waendelee kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kuratibu utoaji wa misaada kwenye maeneo yaliyoathirika.

“Barabara ya Mkongo hadi Utete na ile ya kutoka Mloka Mkongo zote zimeathirika. Tunafanya kazi ya kurejesha mawasiliano ili wananchi waweze kupata huduma muhimu,” amesema.

Read more: Ministers Survey Flood Damage In Rufiji And Kibiti

https://mediawireexpress.co.tz/ministers-survey-flood-damage-in-rufiji-and-kibiti/

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo jioni (Jumanne, Aprili 16, 2024) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Chumbi, wilayani Rufiji, mkoani Pwani ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko kwenye eneo hilo. Hadi sasa waathirika 740 wako kambini.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Ikwiriri, Rufiji akitokea Mlimba, Morogoro aliwaomba wananchi hao waendelee kutulia kwani serikali iko nao na itaendelea kuwahudumia hadi hali yao irejee katika hali ya kawaida.

“Naomba mpokee salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunatambua kuna watu wamepoteza mali na wengine mifugo,” amesema.

Amewataka watendaji wa vijiji waendelee kubaini maeneo mapya ya kuishi ambayo yatatumika kuhamisha kaya zilizoathirika. “Watendaji wa vijiji tuainishe maeneo mapya ya kwenye miinuko ili baadaye watu waweze kuhamishiwa huko,” amesema.

Read more: Serikali yaja na mwarobaini mafuriko ya Rufiji

https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/serikali-yaja-na-mwarobaini-mafuriko-ya-rufiji-4590304

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza TARURA, TANROADS na TAZARA zishirikiane kufanya ukarabati katika maeneo yote yaliyopata athari wakati Serikali inasubiri kumalizika kwa mvua ili iweze kufanya ukarabati mkubwa.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi (OWM-SBU), Ummy Nderiananga, Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi na watendaji wengine.

Author

3 Comments

  1. I carry on listening to the news update talk about getting boundless online grant applications so I have been looking around for the top site to get one. Could you tell me please, where could i acquire some?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

ICC Prosecutor Khan Faces Retaliation Allegations Amid Inquiry

U.N. investigators are probing allegations of sexual misconduct against Karim

Dar Official Condemns Woman’s Abuse, Pledges Support

The Regional Commissioner of Dar Es Salaam, Albert Chalamila, has