Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Kura ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2024/25: Utata na Matumaini

Mjadala ulikuwa mkali, huku hoja mbalimbali zikiibuka, ikiwemo suala la upungufu wa sukari nchini, uwekaji tozo kwenye gesi ya magari, kikokotoo na hali ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ubadhirifu wa mali za umma,
June 26, 2024
by

Bunge la Tanzania linatarajia kupiga kura ya wazi leo, ambayo itaamua hatma ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25. Zoezi hili la kupiga kura linafuata siku saba za majadiliano juu ya bajeti hiyo, ambayo iliwasilishwa bungeni Dodoma Juni 13 mwaka huu.

Wabunge wataitwa mmoja mmoja kupiga kura ya NDIYO, HAPANA au KUTOKUAMUA. Hii ni bajeti ya nne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mjadala ulikuwa mkali, huku hoja mbalimbali zikiibuka, ikiwemo suala la upungufu wa sukari nchini, uwekaji tozo kwenye gesi ya magari, kikokotoo na hali ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ubadhirifu wa mali za umma, ubovu wa barabara na madeni ya wakandarasi pamoja na ugumu wa upatikanaji wa dola.

SomaZaidi;Deni la Serikali Linafikia Trilioni 91.7

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo watazipatia majibu hoja hizo kabla ya zoezi la upigaji kura kuanza.

Baada ya kupiga kura, kura hizo zitahesabiwa na uamuzi wa bajeti hiyo utatolewa endapo imepitishwa ama la. Ikiwa Bunge litakataa kupitisha bajeti iliyopendekeza na Serikali, Rais atalivunja kwa mujibu wa Katiba.

Author

2 Comments

  1. I don’t even know how I finished up here, however I believed this publish was once good. I don’t understand who you might be but certainly you’re going to a famous blogger if you are not already 😉 Cheers!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Zelensky Predicts Putin’s Rule Will End Soon

 Ukrainian President Volodymyr Zelensky has made a bold statement about

House Panel Publishes Epstein Files Amid Transparency Demands

The U.S. House Oversight Committee has released more than 33,000