Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Waziri wa Afya aagiza hospitali zote za rufaa kutoa huduma ya kemo

Tiba Kemia hutolewa katika Hospital ya Rufaa ya  Muhimbili na Ocean Road tu na wagonjwa wamekuwa wengi kote nchini hivyo ni wakati wa Hospital za Rufaa za Mikoa kutoa huduma hiyo lengo ni kuwapunguzia usumbufu wagonjwa.
December 30, 2023
by

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameagiza Hospital zote za Mikoa za Rufaa nchini kuhakikisha zinatoa Tiba Kemia lengo ni kumpunguzia mgonjwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mwalimu alisema hayo leo Jijini Arusha mara baada ya kutembelea Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kuzindua maabara ya kisasa ya hospital hiyo na kusema kuwa Tiba Kemia hutolewa katika Hospital ya Rufaa ya  Muhimbili na Ocean Road tu na wagonjwa wamekuwa wengi kote nchini hivyo ni wakati wa Hospital za Rufaa za Mikoa kutoa huduma hiyo lengo ni kuwapunguzia usumbufu wagonjwa.

Waziri huyo alisema hatua iliyofanywa na Hospital ya Rufaa ya Mount Meru Mkoani Arusha ya kutaka kuanzisha huduma ya Tiba Kemia ameiunga mkono na kuzitaka hospital nyingine za Rufaa za Mikoa kuiga mfano wa hospital hiyo.

Waziri aliusifu uongozi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru chini ya Mganga Mfawidhi Dkt Alex Ernest kwa usafi,utoaji wa huduma safi na uwepo wa dawa na vifaa tiba na na  Utendaji kazi na usimamizi wa dhati kwa watumishi na kutoa huduma kwa wananchi na kusema kuwa hospital nyingine zinapaswa kuiga mfano huo.

Waziri wa Afya Tanzania, Ummy Mwalimu

Alisema Dkt Alex ni mfano wa madaktari Bingwa kote nchini kwani yuko karibu na watumishi wote wa hospital hiyo na anatatua changamotozao zote hivyo Madaktari wengine wa Hospital za Rufaa wanapaswa kuiga mfano.

‘’Nimeridhishwa na usafi na utoaji huduma katika Hospital hii ya Mount Meru kwani nimejionea mwenyewe na mnastahili pongezi na msibweteke hakikisheni mnaongeza kasi kwa maslahi ya wananchi’’alisema Mwalimu.

”Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hatudai kwani emashafanya kazi yake ya kutoa fedha katika huduma ya Afya mamilioni ya fedha kote nchini hivyo ni wajibu wetu kutoa huduma safi kwa wananchi”alisema

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Dkt Charles Mkombachepa alimweleza Waziri kuwa Mkoa wa Arusha kwa sasa una vituo vya afya 431 hadi disemba mwaka huu na serikali inamiliki vituo 259 sawa na asilimia 60 ukilinganisha na mwaka 2021/22 ambapo kulikuwa na vituo 241 sawa na asilimia 57 na taasisi za dini na binafsi zinamiliki vituo vya afya 172 sawa na asilimia 39.

Dkt Mkombachepa alisema kuwa kuna hatua kubwa sana imepigwa katika kujenga na kuimarisha miundambinu ya kutolea huduma ya afya kwani katika 2021/22 kulikuwa na hospital 6 za Halmashauri na kufikia Disemba mwaka huu Halmashauri zote saba Mkoani Arusha zina Hospital na zote zimeanza kutoa huduma.

Alisema mwak 2021/22 kulikuwa na vituo vya afya 37 na mwaka 2023/24 jumla ya vituo afya 3 vimeongezwa na kufikia 40,mwaka 2021/22 kulikuwa na zahanati 194 na mwaka 2023/24 zimeongezeka na kufikia zahanati 211,mwaka 2021/22 kulikuwa na vyumba vya upasuaji 17 ukilinganisha na mwaka 2023/24 kuna vyumba vya upasuaji 21 kwa vituo vya serikali.

Naye Mganga Mfawidhi Alex Ernest alimweleza Waziri Mwalimu kuwa Hospital ya Rufaa ya Mount Meru inanunuwa dawa MSD kwa fedha taslimu,wazabuni na wafanyakazi wa Hospital hiyo hawana deni nao kwa kuwa kila kitu wanachostahili kulipwa wameshalipwa au wanalipwa kwa wakati.

Author

44 Comments

  1. Howdy! I know this is kinda off topic nevertheless I’d figured I’d ask.
    Would you be interested in exchanging links or maybe guest writing a blog post or vice-versa?
    My website discusses a lot of the same topics as
    yours and I think we could greatly benefit from each other.
    If you might be interested feel free to send me an e-mail.
    I look forward to hearing from you! Great blog by the way!

  2. Amazing blog! Do you have any recommendations for aspiring writers?
    I’m hoping to start my own website soon but I’m a little lost on everything.
    Would you advise starting with a free platform like WordPress or go for a paid option? There are so many choices out there that I’m completely
    confused .. Any ideas? Bless you!

  3. I’m truly enjoying the design and layout of your website.

    It’s a very easy on the eyes which makes it much more
    pleasant for me to come here and visit more often. Did you hire out a designer to create your theme?
    Outstanding work!

  4. Hey there, I think your site might be having browser compatibility issues.
    When I look at your blog in Ie, it looks fine but when opening in Internet Explorer, it has some overlapping.
    I just wanted to give you a quick heads up!
    Other then that, amazing blog!

  5. I do not know if it’s just me or if perhaps everyone else experiencing issues with your blog.
    It appears like some of the written text within your
    content are running off the screen. Can someone else please provide feedback and
    let me know if this is happening to them too? This may be a problem with my internet browser because I’ve had this happen previously.
    Thank you

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania-Zanzibar Committee Addresses Union Issues

The joint committee meeting between the Government of the United

WhatsApp to Discontinue Service on Older Devices

WhatsApp has announced that it will discontinue its service on