Dark
Light

Rais Samia Atoa Fedha Za Dharura Wizara Ya Ujenzi

Bashungwa amemuelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam kufika katika barabara hiyo na kufanya tathimini ya maeneo yote yaliyoribika ili kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanaendelea kuwepo wakati wote.
April 15, 2024
by

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia Wizara ya Ujenzi fedha za dharura ili kusaidia kufanya ukarabati kwenye maeneo ambayo mawasiliano ya barabara yamekatika kutokana na mvua za El-Nino zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

Bashungwa ameeleza hayo Bungeni jijini Dodoma leo Aprili 15, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile aliyehoji kuhusu Mkakati wa muda mfupi wa kukarabati barabara ya Gomvu – Kimbiji – Pembamnazi ili iweze kupitika kwa gharama nafuu.

Read More: Wanaosimamia Ujenzi Barabara Ya Kibaoni Kuondolewa

https://mediawireexpress.co.tz/wanaosimamia-ujenzi-barabara-ya-kibaoni-kuondolewa/

Akijibu swali hilo, Bashungwa amemuelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam kufika katika barabara hiyo na kufanya tathimini ya maeneo yote yaliyoribika ili kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanaendelea kuwepo wakati wote.

Bashungwa amefafanua kuwa barabara ya Gomvu – Kimbiji – Pembamnazi ni sehemu ya barabara ya Mjimwema – Kimbiji – Pembamnazi yenye urefu wa kilometa 49 ambayo inajengwa kwa awamu kwa kiwango cha lami kulingana na upatikanaji wa fedha.

“Kwa sehemu ya Cheka – Avic (km 2) tayari ujenzi umekamilika, Kwa sehemu ya Avic – Kimbiji (km 10) taratibu za manunuzi ya kumpata Mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi zinaendelea. Aidha, ujenzi kwa sehemu iliyobaki ya Kimbiji hadi Pembamnazi itajengwa kulinganana upatikanaji wa fedha”, amefafanua Bashungwa.

Read More: Ujenzi Wa Barabara Ya Sanzate-Nata Wafikia 45%

https://mediawireexpress.co.tz/ujenzi-wa-barabara-ya-sanzate-nata-wafikia-45/

Kuhusu utekelezaji wa barabara ya Kibada – Mwasonga (km 41), Bashungwa amemuelekeza Mkandarasi kuanza kufanya maandalizi ya ujenzi katika eneo la mradi (Mobilization) wakati akiandaliwa taratibu za malipo ya awali pamoja na kuwajibika kuendelea kufanya matengenezo ya barabara kwasababu ashakabidhiwa barabara hiyo.

6 Comments

  1. I truly wanted to type a brief message to thank you for the unique solutions you are giving on this site. My prolonged internet investigation has at the end of the day been compensated with good know-how to write about with my close friends. I would state that that many of us visitors actually are unquestionably fortunate to exist in a notable community with many lovely professionals with interesting suggestions. I feel extremely happy to have come across your web pages and look forward to plenty of more excellent moments reading here. Thank you again for a lot of things.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

AZAM: Two Clubs Want To Sign Dube

Azam have admitted receiving offers from Simba and Sudan’s giants

Trump’s Executive Order Bans Skinny Jeans for Men

 President Donald Trump has signed an executive order that has