Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Wananchi Watakiwa Kuweka Akiba Sehemu Salama

Bw. Bakari alisema akiba inaweza kuhifadhiwa Benki, Vikundi au SACCOS zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria.
June 9, 2024
by

Serikali imewataka wananchi kuweka akiba ya fedha zao kwa kuwa akiba ni sehemu mojawapo ya mapato ambayo mwananchi, mfanyabiashara au mjasiriamali anaweza kuhifadhi sehemu salama kwa ajili ya kutimiza malengo aliyojiwekea.

Akitoa Elimu kwa Wananchi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Afisa uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Bw. Omar Bakari, alisema ni muhimu kuwa na fedha ya dharura ambayo itasaidia wakati litakapotokea tukio lisilotarajiwa.


“Tunaposema tukio la dharura ni kama ajali, misiba, kupoteza kazi, msimu wa njaa na mazingira mengine ambayo hayakutarajiwa.” Alisema Bw. Bakari

Bw. Bakari alisema akiba inaweza kuhifadhiwa Benki, Vikundi au SACCOS zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Soma Zaidi: Walimu Biharamulo Wapewa Elimu ya Fedha

Aidha, Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Winfred Mwamkalaba, alisema kuwa baadhi ya wakazi wa Sumbawanga walizoea kufanya mambo kwa mazoea lakini baada ya huo mfumo wa Huduma Ndogo za Fedha kuanzishwa na kutoa elimu na kuwepo kwa waratibu walioko kwenye halmashauri zingine za mkoa wa Rukwa, imeamsha ari na wengi wanajitokeza kusajili vikundi vyao.

“Nitoe wito kwa wananchi wengine ambao wanafanya shughuli zao bila kusajiliwa wafike Ofisi za Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga au wataalamu kutoka kwenye kata ambao wanafanya kazi hizo kwa ajili ya kuwapa miongozo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kusajili vikundi vyao.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Nigerian lawmakers pass 2024 budget after Tinubu seeks extra funds

Nigerian lawmakers approved a 28.77 trillion naira ($34 billion) budget

Natural Gas Drives Development In Songosongo

Residents of Songo Songo Ward in Kilwa District, Lindi Region