Breaking News
Breaking News
Dark
Light

RC Makonda Adai Mawaziri Wanawalipa Watu Kumtukana Rais

"Wapo watu wanaotumia fedha kuwaagiza watu kumtukana Rais Samia, naomba waache mara moja, ninawafahamu kwa majina, msipoacha Jumatatu nitawataja, wapo hadi mawaziri."
April 12, 2024
by

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka watu wanaotumia fedha kuwatuma watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan mtandaoni kuacha mara moja na endapo wataendelea, Jumatatu ya Aprili 15,2024 atawajata.

Makonda amesema, “Wapo watu wanaotumia fedha kuwaagiza watu kumtukana Rais Samia, naomba waache mara moja, ninawafahamu kwa majina, msipoacha Jumatatu nitawataja, wapo hadi mawaziri.”

Makonda amesema hayo leo Aprili 12, 2024 kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine yaliyofanyika Monduli mkoani Arusha.

Read: Makonda hints Possibility of Monthly Public Audience with Samia

https://mediawireexpress.co.tz/makonda-hints-possibility-of-monthly-public-audience-with-samia/

“Ni jambo la kusikitisha kwa baadhi ya viongozi kutotambua dhamana walizonazo…badala ya kuleta utulivu na maelewano kati ya serikali na jamii, wanatumia nafasi zao kuleta uchonganishi kati ya jamii na serikali…” – Rais Samia Suluhu Hassan akiwasihi viongozi walioteuliwa kutumia dhamana za nafasi walizopewa kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao.

Rais Samia  ametoa pole kwa wananchi wate waliopatwa na athari za mafuriko pamoja na ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya msingi Ghati Memorial ya jijini Arusha iliyotokea leo baada ya kusombwa na maji katika eneo la Engosengiu kutokana na uzembe wa dereva na kusababisha vifo vya wanafunzi watano.

Read: Makonda Umechangamsha Chama ,Nakuamini-Rais Samia

https://mediawireexpress.co.tz/makonda-umechangamsha-chama-nakuamini-rais-samia/

Amewataka pia wananchi kuchukua tahadhari juu ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Author

4 Comments

  1. whoah this blog is wonderful i love reading your articles. Keep up the great work! You know, lots of people are looking around for this info, you can aid them greatly.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

China Launches Gold ATM That Melts and Pays Instantly

China has unveiled the world’s first gold ATM that can

The “New world Order”…is Russia slowly emerging global Giant?

Since 2017, the world has been living through a period