Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Makalla Awahakikishia CCM Upele Umepata Mkunaji

“Lazima tupate ushindi na kwa mwakani fomu ni moja ya Rais Samia Suluhu Hassan, Uchaguzi ni kura, uchaguzi ni namba bila Wanachama walioandaliwa huwezi kushinda Uchaguzi ndio maana tutakuja huko kueleza mazuri yaliyofanywa na CCM , niwaombe Wana CCM kipokeeni Chama ili tufanikishe Uchaguzi”
April 5, 2024
by

Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu. Amos Makalla amewataka Wanachama wa CCM waamini wanae Mwenezi na wasiwe na wasiwasi huku akisema yupo tayari kwa mdahalalo wowote kujibu hoja na kushindana kwa hoja na sio vihoja na kusisitiza kuwa upele umempata Mkunaji.
Makalla Amesema hayo wakati wa hafla fupi ya Mapokezi  ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifailiyofanyika leo tarehe 5 Aprili, 2024 Katika uwanja wa nje wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam iliyopo Lumumba.

“Ninaposema nimerudi nyumbani naelewa majukumu ya Katibu wa Uenezi wa CCM maana nasoma mitandaoni baadhi wananikumbusha majukumu nawaambia nayaelewa yapo kwenye Katiba ya CCM, Ibara ya 107 kifungu cha pili A hadi F, leo mnatupokea Sekretarieti yetu imeundwa, nataka niwahakikishie Timu imekamilika”

Read>> http://Watanzania Wanajivunia Uongozi Wa Rais Samia- Dkt. Nchimbi

“Uzuri tunajuana, Boss wetu tunamuheshimu kwasababu ametuongoza, ametutengeneza, ingekuwa kuingia Jeshini namba yake inasoma ya kwanza, tutafanya kazi kwa bidii na kukiletea Chama ushindi, msingi wa Chama chochote cha siasa ni kushika dola, na ukitaka ushinde vizuri Uchaguzi Mkuu lazima upate ushindi mzuri Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kazi yetu sasa tunarudi kwa Wanachama wa kawaida na Wananchi chini, tutalala huko tutapiga kambi lazima kieleweke”

“Lazima tupate ushindi na kwa mwakani fomu ni moja ya Rais Samia Suluhu Hassan, Uchaguzi ni kura, uchaguzi ni namba bila Wanachama walioandaliwa huwezi kushinda Uchaguzi ndio maana tutakuja huko kueleza mazuri yaliyofanywa na CCM , niwaombe Wana CCM kipokeeni Chama ili tufanikishe Uchaguzi”

Read>> https://mediawireexpress.co.tz/muziki-umeanza-hii-safu-ni-ujumbe-tosha-mongella/

“Mimi nimezaliwa hapa Dar es salaam Ocean Road, nimekulia Kilwa Road Baba Polisi, Mama Polisi, nimekulia kwenye Chama tawi la Kawe, tupo tayari kufanya siasa za kistaarabu na kujibu kwa hoja, muamini mnae Katibu Mwenezi msiwe na wasiwasi nipo tayari kwa mdahalo wowote kujibu hoja bila wasiwasi, nataka kuwaambia upele umepata Mkunaji, nipo tayari kwa siasa za maridhiano, tushindane kwa hoja sio kwa vihoja, kwa vihoja sipo tayari lakini kwa hoja nipo tayari”

Author

5 Comments

  1. What¦s Happening i am new to this, I stumbled upon this I have found It absolutely useful and it has aided me out loads. I’m hoping to give a contribution & assist other customers like its helped me. Great job.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Jeff Bezos Regains Title of World’s Richest Man, Surpassing Elon Musk

Jeff Bezos has dethroned Elon Musk to reclaim his title

Zanzibar To Launch National Campaign for Child Protection

The National Campaign “#MtotoNiMboniYangu,” which translates to “A Child is