Dark
Light

Yanga SC Yatuma Malalamiko CAF Kudhulumiwa Goli

Klabu ya Yanga SC imeandika barua ya malalamiko kwa CAF kufuatia kukataliwa kwa goli la Azizi Ki dakika ya 57 dhidi ya Mamelodi Sundowns katika michuano ya CAF Champions League hatua ya robo fainali, Refa wa mchezo huo Raia wa Mauritania, Dehane Beida kutokwenda kujiridhisha kupitia VAR.
April 6, 2024
by

Hivyo Yanga imeiandika kupitia kwa Mkurugenzi wake wa sheria Simon Patrick, imewalalamikia Marefa kwa kushindwa kutumia teknolojia ya VAR kupata ufumbuzi, hivyo wanaamini na kulalamika kupitia sheria namba XVI kwamba kuna viashiria vya upangaji wa matokeo ikiwemo pia kitendo cha Refa wa kati kushindwa kwenda kwenye VAR kuangalia utata wa goli hilo licha ya kwamba aliweza kwenda kwenye VAR kuhakiki faulu ya Mchezaji wa Yanga.
Pia pamoja na mambo mengine Yanga wameiomba CAF ichunguze tukio hilo kwa undani kwa kutumia ushahidi wa rekodi za VAR na footage za mechi ili kubaini endapo kuna viashiria vya upendeleo kwa Mamelodi vimefanyika na ikijiridhisha kuna upendeleo ichukue hatua kwa kila aliyehusika, iweke hatua madhubuti za kudhibiti tukio kama hilolisijirudie kwenye mechi zijazo na pia ichukue maamuzi mengine ambayo CAF itaona yanafaa chini sheria za mpira za CAF namba XVI kifungu namba 3.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania Ports Register Major Gains After Reforms

Tanzania’s maritime sector is experiencing a robust transformation, with the

Religious Leaders Urge Dialogue Over Planned Protests

leaders from the Twariga Islamic Organization in Arusha have expressed