Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Tsh Trilioni 44.19 Zaombwa Na Wizara Ya Fedha

June 4, 2024
by

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuiidhinishia wizara yake makadirio ya mapato na matumizi ya kiasi cha Shilingi trilioni 44.19, kati ya makadirio ya Shilingi trilioni 49.35 za Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2024/2025 ili iweze kutekeleza vipaumbele vyake vitano ilivyopanga kuvitekeleza katika mwaka wa fedha 2024/2025

Ameeleza kuwa kati ya kiasi hicho kinachoombwa Shilingi trilioni 29.42 zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Misaada na mikopo inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 5.13, mikopo ya kibiashara kutoka nje na ndani ya nchi inakadiriwa kuwa Shilingi trilioni 9.60 na maduhuli ni Shilingi bilioni 45.01.

Soma Zaidi:Nchemba Awahakikishia Wafanyabiashara Usalama wa Kodi

“kwa mwaka 2024/25, Wizara ya Fedha inaomba kuidhinishiwa matumizi ya jumla ya Shilingi trilioni 18.17 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mafungu nane (8) ya kibajeti. Kati ya kiasi hicho, Shilingi trilioni 17.63 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikijumuisha huduma ya deni la Serikali shilingi trilioni 13.13, mishahara Shilingi bilioni 946.45, matumizi mengineyo Shilingi bilioni 937.30 kwa mafungu ya wizara na taasisi zake, Huduma za Mfuko Mkuu Shilingi trilioni 2.61 na matumizi ya maendeleo Shilingi bilioni 544.05” Amesema Dkt. Nchemba.

Aidha ameliomba Bunge kuidhinisha pia bajeti ya Fungu 045 linalohusisha Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi iidhinishiwe jumla ya shilingi bilioni 112.73 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya kiasi hicho, Shilingi bilioni 101.26 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 11.47 matumizi ya maendeleo.

Amevitaja vipaumbele vitano vya mafungu ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2024/25 kuwa ni pamoja na kutafuta na kukusanya mapato ya shilingi trilioni 44.19 kati ya maoteo ya Shilingi trilioni 49. 35 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Serikali, Kuimarisha na kusimamia mifumo ya mapato, matumizi na mali za Serikali ikiwemo IDRAS, TANCIS, MUSE, NeST, CBMS na GAMIS na kuhudumia deni la Serikali kwa wakati na kuboresha kanzidata ya kutunza taarifa za deni.

Dkt. Nchemba amevitaja vipaumbele vingine kuwa ni kutoa elimu ya huduma za fedha kwa wananchi kwa lengo la kukuza huduma jumuishi za fedha nchini.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

China Unveils Zuchongzhi-3, A Quantum Computing Breakthrough

China has introduced a groundbreaking quantum computer, Zuchongzhi-3, which researchers

Zelenskyy Meets Ramaphosa In First South Africa Visit

Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy was warmly welcomed by South African