Breaking News
Breaking News
Dark
Light

TANESCO: “Umeme Umekatika Baada Ya Hitilafu Gridi Ya Taifa”

TANESCO imeeleza baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dodoma na Iringa Huduma imeanza kurejea huku Wataalamu wao wakiendelea na jitihada za marekebisho ili kurejesha Huduma hiyo Maeneo mengine
May 4, 2024
by

 Baada ya maeneo mengi Nchini kukosa Huduma ya Umeme kuanzia usiku wa kuamkia leo Mei 4, 2024, Shirika la Umeme Tanzania [TANESCO] limesema hali hiyo imesababishwa na hitilafu kwenye Mfumo wa Gridi ya Taifa iliyotokea majira ya Saa 8:40 Usiku

TANESCO imeeleza baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dodoma na Iringa Huduma imeanza kurejea huku Wataalamu wao wakiendelea na jitihada za marekebisho ili kurejesha Huduma hiyo Maeneo mengine

Soma Zaidi:TANESCO Gets New Board of Directors to Address Country’s Power Crisis

Nukuu ya Taarifa kwa Uma iliyo tolewa na shirika hilo ni ” Shirika la Umeme Tanzania [TANESCO] linawataarifu wake kuwa hitilafu iliyojitokeza katika mfumo wa gridi ya taifa imefanywa kazi na wataalamu wetu

Mpaka sasa huduma ya umeme imerejeshwa kupitia vituo vyetu vya kupokea, kupoozea na kusambaza umeme Nchini na tayari maeneo mengi yanapata huduma

Shirika linawashukuru wateja wake wote kwa uvumilivu katika kipindi chote ambacho huduma hii ilikosekana”

Awali kabla ya taarifa hiyo, Shirika hilo lilitoa taarifa ya kukosekana kwa umeme katika baadhi ya maeneo, huku ikithibisha kuwepo kwa jitihada ya wataalamu kufanyia kazi hitilafu hiyo na kuhakikisha umeme unarudi katika maeneo yote.

Author

6 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Pamba FC Yarudi Ligi Kuu, Wadau Waishauri Isipotee

Ligi kuu ya NBC Tanzania bara itampokea mgeni aliyepotea kwa

Government Strengthens Efforts to Control Dangerous Wildlife

President Samia Suluhu Hassan has reaffirmed the government’s commitment to